Kama wewe ni mtu wa masoko bila shaka utakuwa unaelewa kuwa sio kazi rahisi kumbadilisha mtu anayetembelea biashara yako kuwa mteja rasmi. Katika kutengeneza wateja, vipo vikwazo vinavyoweza kuzuia mtu anayetembelea ukurasa wako ashindwe kujaza fomu kwenye tovuti yako kupata taarifa zake kama mteja.

Hivyo basi ukiwa kama mtu wa masoko moja ya lengo lako kubwa ni kutengeneza njia ambayo itaondoa msuguano wowote kwa ajili ya kutengeneza wateja. Hili kufanikiwa unahitaji kuondoa usumbufu na vizuizi vinavyomchanganya mteja.

SOMA ZAIDI: 

 

Njia 7 za kuondoa vizuizi mtandaoni ili kutengeneza wateja kwa ufanisi.

1.Fupisha ukurasa wako wa kumvutia mteja (Lead Capture form)

Ukurasa wa mteja ndio sehemu lengwa ya kumvuta na kumshawishi mteja. Lengo maridhawa la ukurasa huu ni kumtaka mteja ajaze taarifa zake kutokana na maudhui aliyoyapitia kwenye ukurasa husika. Inakusaidia kutengeneza wateja kwa ufanisi

Urefu na ufupi wa fomu unatumika katika kupata idadi na ubora wa taarifa za kwenye ukurasa wa mteja. Fomu inavyokuwa fupi ndivyo unavyokaribisha wateja wengi zaidi kuacha taarifa zao kwa urahisi. Tofauti na fomu iliyo ndefu. Fomu yenye maelezo machache itakupa idadi ya wateja wengi licha ya kuwa haitakupa taarifa zilizo bora lakini ni rafiki katika kutengeneza wateja.

2.Tengeneza ukurasa wa kumvutia mteja wenye lengo moja maalumu.

Ukurasa wa kumvutia mteja ndio sehemu pekee inayotengeneza matangazo ya biashara husika na ndio sehemu ya kutengeneza wateja.

Jinsi unavyoufanya ukurasa wako kuwa wa biashara moja husika au lengo moja husika ndivyo utakavyovutia wateja wengi zaidi. Tunategemea wateja wakatapokuwa wanahitaji bidhaa au huduma fulani wanajua wapi wataipata.

3.Ondoa viongoza tovuti vilivyopo Juu, chini na pembeni.

Kila tovuti ina viongoza tovuti vyake. Viongoza tovuti ndivyo vinavyomuongoza mtu anayetembelea tovuti kwa ajili ya huduma Fulani. Utumika kumuhamisha mteja kutoka ukurasa mmoja kwenda mwingine kwa kiunganishi maalumu cha huduma husika kupitia mtandao. Hii pia itakusaidia kutengeneza wateja.

Ondoa viongoza tovuti (Website navigation) vilivyopo pembeni, juu na chini ili kumfanya mteja anayekuja kwenye ukurasa wako aendelee kubaki kutokana na kutokuwa na chaguzi nyingi kwenye ukurasa wako. Hii itasaidia kuwavuta watu wengi kuendelea kubaki na kuweza kutengeneza wateja.

4.Epuka kuonyesha ofa nyingine kwenye ukurasa wa mteja.

Kwakuwa umeondoa viongoza tovuti ulivyoelekezwa kwenye tovuti yako hakikisha kuwa haumchanganyi tena mteja. Hakikisha unaitangaza ofa yako uliyokuwa umeilenga. Usimchanganye mteja kwa kuitangaza ofa nyingine.

kama unahitaji kutengeneza wateja weka macho yako kwenye hiyo ofa pia weka macho yako kwa mteja ili asipate nafasi ya kufikiria kwenda sehemu nyingine.

5.Tengeneza CTA yenye mashiko kwa ajili ya tovuti yako.

Kama mtu wa masoko usilenge tu sana kwenye kutangaza ofa bali jitahidi kumshawishi mtu anayetembelea kwa mara ya kwanza ili avutiwe na bidhaa au huduma yako. Hii itakusaidia kutengeneza wateja wengi zaidi.

Njia nzuri ya kufanikiwa hili ni kuweka ujumbe unaomshawishi mteja afanye maamuzi kwenye bidhaa au huduma yako (Call To Action) kwenye tovuti yako na hata blogu. kwa kufanya hivi utaweza kutengeneza wateja kwa wingi.

6.Gawa ujumbe wako wa kumshawishi mteja kwenye mitandao ya kijamii.

Mitandao ya kijamii inachukuwa watumiaji wengi sana ulimwenguni. Mitandao ya kijamii ni njia maridhawa ya kutengeneza wateja wa baishara yako.

Kwakuwa watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wanaweza wasiwepo kwenye tovuti yako. Unapaswa kutengeneza hatua chache za kumshawishi mteja wa aina hiyo.

Tovuti Mpya

7.Tumia lughya ya vitendo kutengeneza wateja

Kama unahitaji kutengeneza wateja kwa wingi, unatakiwa kumueleza mteja anayekuja kwa mara ya kwanza ni nini cha kufanya. Kutumia lugha ambayo ni ya vitendo.

Mfano unaweza kumuambia mteja “Pakua vitabu mtandaoni hapa” “Jisajili na webiner leo”

Kumbuka unapomrahisishia mteja kuingia kwa urahisi kwenye tovuti yako kunatoa nafasi kubwa ya kupata mzunguko mkubwa na ukusaidia kutengeneza wateja. Hili kuweza kupata tovuti yenye kuuza kwa mteja BONYEZA HAPA.