Kukua kwa kasi kwa technologia ya ya kidigitali kumerahisisha sana utangazaji na upatikanaji wa Ajira Tanzania.

Miaka ya nyuma ilikuwa ni lazima kununua Gazeti kila siku, na sio Moja  bali mengi ili kuweza kujua nafasi za Kazi zilizotangazwa kwa siku hiyo kupitia magazeti hayo.Magazeti ya kitanzania ambayo ni maarufu hadi leo hii katika kutangaza nafasi ajira ni kama yafuatayo;

  • Daily News
  • The Gurdian
  • The Citizen
  • Citizen
  • Others

Kwa sasa mambo yamekuwa marahisi sana kulinganisha na miaka ya nyuma. Unaweza kupata matangazo ya kazi kwa urahisi kwa kutumia Internet bila hata ya kununua pisi la Gazeti.

Pia imepunguza gharama kwa kiasi kikubwa sana. Unahitaji gharama ndogo tu kwa ajili ya kukuunganisha na mtandao tu kuliko kununua magazeti hata matano.

Je wajua Tovuti ambazo  zinazotoa Matangazo ya Ajira katika Sector mbalimbali? Kama Vile Kilimo, Biashara, Sayansi na Technologia, Uvuvi n.k

Zifuatazo ni Tovuti 5 Bora Zinazoweka Matangazo ya Ajira;

  1. Brighter Monday- brightermonday.co.tz

Ni moja ya tovuti bora unapokuja kwenye swala la kutafuta kazi. Mwonekano tu wa tovuti unakupa uhakika wa kitu ambacho unakitafuta.

Ni tovuti inayotangaza nafasi za kazi katika nchi za Africa mashariki. Ilianzishwa 2006 nchini Kenya, Nia na madhumuni yake yakiwa kukuza soko La Ajira kwa Nchi za Africa mashariki.

Tovuti hii imerahisisha namna ya kupata kazi unayoitafuta kwa kuweka Filter ambazo zinakusaidia kutafuta kazi kwa ;

  • Kuchagua mahali au sehemu(location) kazi ilipo
  • Kuchagua Category au Sector ya kazi kwa mfano  Kilimo, uvuvi, Technologia n.k
  • Kuandika kile unachokitafuta

Pia waweza weka wasifu wako(CV)kwa kampuni zinazotafuta wafanyakazi. Tovuti inakuwezesha kufanya usajili ili kuweza kupata taarifa fupi pale kazi mpya zinapotangwaza.

  1. Ajira Zetu-ajirazetu.co.tz

Tovuti hii inaweka  matangazo ya  kazi kwa Niaba ya Mwajiri au mawakala wa Ajira. Pia ni mojawapo ya Tovuti Bora zinazowawezesha watafuta Kazi/Ajira kuomba nafasi mbalimbali za kazi zilizotangwazwa na tovuti hii.

Ajira Leo Inawawezesha Mwajiri au Mawakala wa ajira kuchagua huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye tovuti kama vile;

  • Job Advertising ,Event/Press Realease
  • Product/Services
  • Business directory listing
  1. Tayoa Employment Portal-vijanatz.com

Vijanatz ni mojawapo ya tovuti bora Tanzania kwa Ajili ya kuwasaidia Vijana kufikia Ndoto zao katika Taaluma walizonazo.Tovuti hii imekuwa msaada mkubwa kwa kuwasaidia Graduate, vijana wasiokuwa na ajira ,Internships na watoa huduma za jamii kufikia malengo yao ya Kitaaluma na ya Kibiashara.

Pia tovuti hii inatoa Training mbalimbali kwa vijana kama vile za;

  • Life Skill
  • Information Communication technology(ICT)
  • Job Search Technique and Support
  • Entrepreneurship Skills
  • Business Development Support
  • Business Plan Development
  1. KaziKazi-kazikazi.co.tz

Tovuti hii inamuunganisha Mwajiri na watu wanaotafuta kazi, Inawawezesha waajiri kupost Nafasi mbalimbali za kazi na pia kwa watafutaji wa kazi kuweka wasifu wao(CV)

Pia inamruhusu mwajiri kulipaia Huduma ya ziada kama anaihitaji. Huduma hizo ni kama vile;

  • Job Listing- mwajiri anaweza kuweka nafasi zote za kazi pamoja na Nembo(logo) na Profile ya kampuni yake katika Tovuti yao
  • Featured Jobs- Wanakupa nafasi wewe kama Mwajiri kuwa Maximum Visibility katika nafasi za kazi ulizozitangaza.
  • Featured Company- Mwajiri anaweza weka nembo(Logo) ya kampuni yake katika Tovuti yao ambapo itampatia High Profile.
  1. Ajira portal- Sekretarieti Ya Ajira- ajira.go tz/portal.ajira.go.tz

Ni tovuti maalumu kwa ajilli ya kuweka matangazo yote ya Ajira zote za Utumishi wa Umma punde zinapotangwaza. Mwajiri anakuwa ni Serikali ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania.

Tovuti hii Inawaruhusu waombaji kuweza kuomba nafasi hizo za kada mbalimbali online. Unaweza kuomba nafasi hizo pale unapokuwa umemaliza kuweka Taarifa zote zinazoitajika kama vile;

  • Kujaza Fomu inayopatikana Mtandaoni
  • Kuweka wasifu wako(CV)
  • Kuweka vyeti vyote Vinavyohitajika n.k

Tovuti zingine ni kama Vile;

  • Jobs in Tanzania- Jobstanzania.net
  • Zoom Tanzania- zoomtanzania.com
  • Ajira Tanzania- ajira.info
  • Ajira Online- ajiraonline.com
  • Kazi Bongo- kazibongo.blogspot.com
  • Jobs(pata Ajira)- jobs.co.tz
  • Nafasi za Ajira- nafasizaajira.com
  • Ajira Kwanza- ajirakwanza.com

kama wewe ni mmoja kati ya watu wanaotafuta kazi(Job Seekers), tovuti Hizi zitakuongoza kuweza kupata kazi ya Taaluma yako Tanzania. Pia kama kuna tovuti zingine ambazo hatujaziweka usisite kutuandikia katika comment, tutaziongeza katika list yetu.