Kila mmoja wetu ni wa tofauti. Hii ni kweli hasa inapokuja kwenye sula la Joto au baridi. Baadhi yetu tuna tabia ya kukimbia hali ya joto, baadhi yetu tunakimbia baridi. Lakini kuna jambo moja tu ambalo karibu sisi sote tunakuwa sawa. Bila kujali hali ya joto hatuwezi kuwa vizuri katika mazingira ya ofisi. Na hata inapokuja bila kujali ya baridi jambo ni lile lile utofauti wake unakuwa ni wa kimazingira.

Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Embr Labs, Sam Shames alisukumwa na mabadiliko ya hali ya joto hasa wanapokuwa maofisini kwa nchi zenye baridi sana kama vile Amerika. Aliamua kutengeneza kifaa au bangili kama ilivyoitwa  kwa ajili ya  kurekebisha joto la mwili.

Bangili hiyo ya Embr (Embr wave) imeingia kwenye maonyesho ya ushuhuda wa vifaa vya umeme (Electronic show) mwaka huu 2019 yaliyofanyika mjini Las Vegas. Ambapo makampuni mbalimbali yamesikika yakipongeza kifaa hicho. Na kusema kuwa teknolojia hiyo imekuja kuboresha ubora wa maisha ya mtumiaji. Na kama ingekuwa kuandika kichwa cha habari basi kingekuwa “ bangili ya kudhibiti Joto”

SOMA ZAIDI:

Bangili ya “Embr wave “ inatumikaje?

Bangili hiyo huvaliwa mkononi na kisha mtumiaji atarekebisha bangili yake kulingana na hali ya joto anayohisi itamsaidia katika mazingira husika. Ina muonekano kama wa saa itakuwa inauzwa madukani kama bidhaa nyingine.

Embr wave ina button za aina mbili, moja ni kwa ajili ya baridi (red button) na nyingine kwa ajili ya joto (blue button).

Sauti ya bangili ndogo kabisa ambayo inaweza kukufanya uhisi joto au baridi katika hali ya joto la wasiwasi kwa dakika chache tu  ni vizuri. Hilo linaweza kuonekana kama aina ya kitu ambacho tunapaswa kukiona ili tuweze kupata uhakika wake.

Vipi kuhusu makampuni mengine yanayotoa huduma kama hiyo?

Sio tu kifaa cha aina yake. Bidhaa za kuvaliwa mwilini kutoka kwenye makampuni mbalimbali kama vile Wizara ya Ugavi, Aircon pamoja na Polar Seal zimeahidi kusaidia kudhibiti joto la mwili bila kujali mazingira.

Huu ni mwendelezo wa matokeo makubwa ya teknolojia mpya. Siku za hivi karibuni tumeona kampuni mbalimbali zikijishughulisha na utengenzajia wa vifaa kama hvi vya kudhibiti joto la mwili. Kampuni ya Polar Seal wao waliamua kutengeneza nguo aina ya jackets zenye uwezo wa kurekebisha joto la mwili.

Maendeleo ya teknolojia yanaenda kwa kasi sana. Uenda na wewe sasa umefikiria njia nyingine kwa ajili ya kuendesha kampuni yako. Deep Media chini ya jopo la wataalamu wa masuala ya IT wanatakaushauri na kukupa njia bora ya kidigitali ili kuweza kuendesha kampuni yako kwa ufanisi zaidi. Bonyeza HAPA kwa mawasiliano