Uwezo wa kutumiana picha pamoja na kushare maoni, matukio na vitu mbalimbali kwa wakati wa sasa ni wazi umebadilisha mfumo maisha. umebadili mfumo wa jinsi gani tunaishi lakini pia umebadilisha mfumo mzima wa ufanyaji wa biashara. Wafanyabiashara wanaoutumia mitandao ya kijamii katika biashara zao uona ndio chanzo cha matokeo chanya katika biashara.

Ni wazi matumizi ya mitandao ya kijamii (Social Media ) ulimwenguni yamekuja na faida kubwa japo yameonekana kuwa na hasara katika nyanja nyingine kwa namna moja ama nyingine.

Mitandao ya kijamii (Social Media) ni nini?

Mitandao ya Kijamii ni jumla ya mkusanyiko wa njia zote za mawasiliano za mtandaoni ikiwalenga jamii husika, katika kushirikiana  kwenye maudhui na mambo mengine yote ya kijamii. Njia hizi ni kama vile Facebook, Instagram, Twitter, WhatsApp, Pinterest, snapchat, Telegram, LinkedIn n.k.

SOMA ZAIDI:

Kulingana na utafiti uliofanywa na mtandao wa kampuni ya Hubspot katika kuimulika mitandao ya kijamii imetoa matokea kadhaa. Hubspot imetumia zaidi ya mwaka mzima wa 2018 kuangalia matarajio ya watuamiaji wa mitandao hiyo kwa mwaka 2019.

Walitumia idadi ya watu zaidi ya 1, 675 kwenye nchi za Canada, Marekani pamoja na Uingereza. Maswali yalikuwa kama ifuatavyo

Qn 1: Ni mtandao upi wa kijamii wanatarajia kuutumia zaidi?

Zaidi ya 52.06% ya waliohojiwa kuwa ni mtandao upi wa kijamii wanatarajia kuutumia zaidi kuliko yote, walijibu kuwa ni Mtandao wa Facebook. Instagram ukapata nafasi ya pili kwa 9.52%. Huku zaidi ya 9.16% ya watu wote waliohojiwa wao hawatatumia kabisa mitandao ya kijamii

Hii inamaanisha kwa mwaka 2019, mtandao wa Facebook utakuwa unazidi kuongeza watuamiaji wake lakini pia kuongeza thamani katika upande wa kibiashara.

Qn 2; Sababu gani zinawafanya waendelee kutumia mitandao ya kijamii 2019?

Waliopoulizwa kuwa ni sababu zipi zinawafanya waendelee kutumia mitandao  kwa mwaka 2019. Wengi zaidi ya 45.54 walijibu kuwa ni sababu tu za maisha binafsi, kuwa karibu na marafiki pamoja na familia.

Utafiti huu unaonyesha wazi kuwa matumizi ya facebook na mitandao mingine inakadiriwa kuongeza watuamiaji wake ambao ndio wateja wetu wa kila siku.

Ni wazi kama mitandao hii itatumiwa vizuri inaweza kuzalisha wateja wengi kwa ajili ya kukuza biashara zetu za kila siku.