Nini Maana Ya Mitandao Ya Kijamii?

Mitandao ya kijamii ni tovuti au mfumo maalumu unaowasaidia au kuwawezesha watumiaji wake kuwasiliana na kutumiana taarifa kwa njia ya meseji, Sauti(audio)  na picha za mnato au mtikisiko(video).

Kupanuka kwa mfumo wa sayansi na Technologia kwa upende wa mawasiliano umeifanya Dunia kuwa kama Kijiji. Pia imesaidia kuwaleta pamoja watu wenye mitizamo inayofanana iwe ya kiuchumi , kisiasa, Kiutamaduni kimichezo n.k .Watu  hao wanaweza wasiliana moja kwa moja kwa kutuma taarifa, habari,picha za aina zote, video na sauti.

Mitandao ya kijamii ikitumiwa vizuri hasa na vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa itasaidia kujenga taifa lililobora kiuchumi.

Je mitandao ya kijamii inakusaidia vipi kuongeza kipato Chako?  

Zifuatazo Ni njia za kukusaidia kukuza kipato kwa kutumia Mitandao ya kijamii;

 

  • Promote jina la Brand yako na Biashara yako

The businessman is working on brand ideas at the desk

Kwa kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, twitter, Blog n.k  inakuwezesha kujitengenezea nafasi nzuri ya kupata wateja wengi kutoka sehemu mbalimbali kutoka mitandao husika. Ni lazima uwajuze watu kuhusu brand yako na biashara yako. Kupitia post zako mbalimbali ni lazima watu waelewe unauza bidhaa gani au unatoa huduma gani.

Kuna namna tofauti ambazo unaweza tumia kukuza jina la Brand  au Biashara yako;

Nazo ni kama zifuatazo:

  • Kupost picha au Video zenye Ubora
  • Tengeneza Nembo(Unique logo) ambayo utaitumia kwenye matangazo yako na post zako zote. Hiyo Nembo itakuwa nikama Kitambulisho chako na cha Bidhaa au huduma zako punde watu wanapoiona.
  • Kutengeneza makala au post zenye Ubora (creative and engaging content)
  • Kutengeneza profile nzuri na inayovutia(Set attractive and Catching profile)
  • Tumia Social Media kuongeza traffic Kwenye Website ya Biashara yako

Kama unamiliki Website unaweza tumia Mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter hata Blog Kuongeza Traffic katika Website yako ambayo itakusaidia wewe Kutokea Juu katika Search Engine pale watu wanapotafuta huduma inayofanana na Keyword katika Website yako.                                  

  • Fanya kazi ya kuwatafutia Kampuni wateja(Affiliate)

Kama haumiliki Biashara au huduma yeyeto lakini Unaushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii pia Unaweza kutumia ushawishi ulionao Kutafutia Kampuni au wafanya Biashara wengine wateja na Ukaongeza kipato chako Kupitia wateja Ambao Unawapelekea. Kwa Mfano unaweza lipwa kwa kupewa asilimia kazaa ya mauzo kutokana na idadi ya wateja uliowapeleka.

  • Uza bidhaa zako mtandaoni

Wafanya Biashara na watoa Huduma wengi sana wamefaidika na matumizi ya mitandao ya kijamii sababu wameitumia kama nguzo mojawapo yakupata masoko(Online Marketing) katika Biashara na huduma wanazozitoa. Wamekuwa wakipata wateja mbalimbali kutokana na kutangaza na kuweka bidhaa zao katika mitandao hiyo.

  • Kuwa na hati Miliki ya video Youtube

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Huu ni moja ya mitandao maarufu sana kwa ajili ya kutazama video. Mtandao huu unakuwezesha kuweka video pengine za kutangaza biashara yako,  bidhaa au huduma ambazo unazitoa na wakati huo huo unaweza kuwa unalipwa kupitia matangazo yatakayokuwa yanatokea katika video  pindi utakapokuwa umeunganisha account yako ya  youtube na ile ya Google Adsense. Pia waweza lipwa kutokana na Idadi ya watu walio tembelea na  kusubscribe katika Account yako .

  •   Mwisho

Watu wengi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuanzia asubuhi hadi jioni na hakuna cha maana anachokifanya. Muda ni mali ukiutumia vibaya utaishia kuwa masikini.