ZINGATIA.

Ustawi na ukuaji wa biashara unahitaji nidhamu kwenye suala la kuamua njia sahihi ya kutengeneza mikakati madhubuti ya kibiashara. Je wewe umeshawahi kufikiri unapitwa na fursa ya kutambua ni jinsi gani unaweza kukuza biashara yako katika kupitia mfumo wa kidigitali? Usihangaike!

Kwa kipindi cha miaka mitano (5) mfululizo kampuni ya masoko ya kidigitali ya Deep media (Deep media Digital Argency) imewekeza katika kutafuta suluhisho la jinsi gani unaweza kuboresha biashara yako na kukuza mauzo kwa zaidi ya 50% kupitia uwanja wa kidigitali.

SOMA ZAIDI:

Kwa kuzingatia mazingira ya kibiashara Deep Media imekuja na huduma ya kibiashara inayojulikana kama Mauzo ChapChap ili kuweza kukuza biashara yako kwa ufanisi.

Kupitia huduma ya Mauzo ChapChap katika kukuza biashara, mteja anaweza,

  • Kuongeza kipato chake kwa zaidi ya 50%
  • Kupeleka biashara yake kwenye Dunia ya mtandao (Tovuti pamoja na mitandao ya kijamii )
  • Kuongeza wateja kutoka kwa watu wa kila siku wanaopitia kurasa zake na kuwatambulisha kwenye bidhaa yake.

Katika utafiti uliofanywa na Deep Media umegundua njia tano au hatua 5 za kukuza biashara yako katika kwa ufanisi pamoja na kuboresha mauzo kwa ziaid ya 50%.

Njia 5 za kukuza biashara na kuboresha mauzo

  1. Kutengeneza Tovuti

Tovuti ndio inayobeba taswira ya biashara au kampuni yeyote ulimwenguni. Hivyo ikiwa hautazingatia utengenezaji bora na sahihi wa tovuti basi utaharibu taswira ya biashara yako. Kabla haujatengeneza tovuti basi fahamu makosa machache ya kuyaepuka wakati wa kutengeneza Tovuti. Ili uweze kuwa na malengo ya kukuza biashara yako kwa ufanisi Tovuti yako ili iwe bora fanya haya,

  • Tengeneza Tovuti inayolipa
  • Unganisha Tovuti yako na mitandao ya kijamii
  • Tengeneza taarifa za kibiashara zenye mashiko
  • Ongeza idadi ya watembeleaji wa ukurasa wako.
  • Wekeza teknolojia ya kisasa ili kuweza kukidhi mahitaji ya muhimu ya watumiaji
  • Tovuti inakuwa na mahitaji muhimu ya biashara yako

2. Jinsi ya kumvutia mteja

Unapoamua kufanya biashara ni wazi au kukuza biashara yako unapaswa kutambua mbinu za kumvutia mteja wako mpya ambaye ndiye mlengwa katika biashara yako.Unaweza kuvutia mteja kutokana na

  • Maudhui utakayoyawasilisha kwenye tovuti yako
  • Kupitia barua pepe
  • Kupitia matangazo ya kibiashara
  • Matumizi ya blogu
  • Mitandao ya kijamii
  • Utoaji wa bidhaa bure (Product trial).
  1. Kufahamu nguvu ya mshindani wako.

Ni vema kufahamu nguvu ya mshindani wako pamoja na kujua vitu gani anafanya kufanya wateja kupenda bidhaa au huduma yake. Kufahamu nguvu ya mshindani wako kunakupa nafasi ya kufanya zaidi ya mshindani wako. Unapaswa kufahamu baadhi ya vitu kama,

  • Udhaifu wa mshindani wako
  • Fahamu jinsi mshindani wako anavyojihusisha na wateja wake.
  1. Kujenga jina la Biashara na uaminifu kwa wateja

Jina la biashara ndio kitambulisho kikubwa cha biashara husika kwa wateja, kwa lugha nyingine ndio jicho la biashara yako linaloweza kutofautisha kati ya biashara yako na biashara nyingine. Deep Media katika kukuza biashara yako inakupa njia baora za kujenga na kukuza jina la baishara yako.

Uaminifu pia katika biashara yako ndio msingi mkubwa katika kukuza biashara. Uaminifu ndio unaotengenza muunganiko wa biashara yako na mteja. Kuna njia nyingi za kutengeneza uaminifu kwa mteja kama vile,

  • Kuzingatia maoni ya mtandaoni hasa kwenye kurasa zako.
  • Onyesha shahidi mbalimbali za wateja waliopata huduma au kununua bidhaa kwako katika njia ya ubora.
  • Pokea mawasiliano ya mteja kwa haraka mara anapotaka kufahamu kitu kutoka kwenye biashara yako.
  1. Ubunifu

Ukiwa kama mmiliki wa biashara siku zote lazima utafute mikakati ya kuboresha na kukuza biashara yako katika hali ya juu zaidi. Ni lazima kutafuta namna ya kutatua matatizo, kuongeza uzalishaji na kuwashinda washindani wako katika soko la biashara. Zipo faida za kuwa mbunifu katika biashara yako zikiwemo,

  • Kukuza biashara yako kwa ufanisi
  • Kupata ubora wa bidhaa yako au huduma unayoitoa
  • Kuwashinda washindani wako

Ukiwa kama mfanyabiashara au unayetarajia kumiliki biashara kwanza lazima utambue kuwa hakuna njia ya kukwepa matumizi ya mtandao au digitali kukuza biashara yako. Deep Media kupitia tafiti zake za kibiashara wanakupa suluhisho la kudumu katika kuboresha biashara yako. Bonyeza HAPA tukusaidie kukuza na kuboresha biashara yako.