Yale mawazo ya kufanya biashara au kazi katika kipindi chote cha maisha yako ni stori sasa. Nchini Marekani zaidi ya raia wake million 30  wanaendesha biashara mtandaoni wakiwa nyumbani kwao.

Wapo ambao wanajiuliza wanawezaje kutumia mtandao kuweza kupata kipato cha ziada kwa kufanya biashara mtandaoni. Lakini wapo ambao wanashindwa kutambua ni biashara zipi wanaweza kufanya kupitia mtandao.

ZINGATIA

  • Tanzania sasa ni soko kubwa la bishara mtandaoni
  • Tanzania ipo kasi kupokea mabadiliko ya teknolojia

Nini maana ya Biashara mtandaoni?

Biashara mtandaoni ni mtindo au aina ya biashara unayoweza kuifanya kupitia mtandao kama njia ya kufanya biashara yako au kutumia mtandao moja kwa moja kujiingizia kipato. Zipo biashara nyingi unazoweza kuzifanya nchini Tanzania kupitia mtandao.

SOMA ZAIDI:  JINSI YA KUINGIZA KIPATO KUPITIA MTANDAO 

Biashara 5 unazoweza kufanya Mtandaoni Tanzania

  • Biashara ya Chakula kupitia magari (Foodtruck)

Unaweza fanya biashara mtandaoni kuuza chakula kupitia kurasa mbalimbali kama vile mitando ya kijamii. Mtu anaweza kutumia Instagramu au Facebook na hata website kuagiza chakula na mfanyabiashara kupitia oda zote za mtandaoni atasambaza chakula chake.

  • Kuendesha mitandao ya kijamii (social media meneja)

Hii ni moja ya biashara mtandaoni inayokuwa kwa kasi sana, watu hujipatia kipato kwa kuziendesha kurasa zote za mitandaoni kupitia makampuni mbalimbali. Unaweza kuanzisha kampuni inayoendesha kurasa mbalimbali za makampuni na kujipatia kipato.

  • Utengenezaji wa Tovuti.

Watu wengi wamejikita sasa katika utengenezaji na ubunifu wa tovuti. Tovuti uwawezesha wafanyabiashara wengi kufanya biashara mtandaoni kupitia biadhaa au huduma wanayoitoa. Unaweza kuwa mmoja wa wabunifu wa tovuti na kujipatia ajira kupitia kazi hiyo.

 

  • Utengenezaji wa picha mjongeo (Video producer)

Nchini Tanzania sasa soko la biashara mtandaoni linakuwa kwa kasi. Idadi a watu wanaotenegeneza video na kuuza mtandaoni inazidi kuongezeka. Biashara ya umiliki wa Youtube chanel sasa imekuwa kubwa. Unaweza tumia Youtube kujipatia kipato.

  • Kuendesha tovuti za makapuni (SEO Consultant)

Je? Unafahamu lolote kuhusu injini pekuzi? Na je una ujuzi wowote wa kuendesha tovuti? Makampuni mengi madogo hawana uelewa wa kibiashara kupitia uendeshaji wa injini pekuzi. Unaweza kutoa elimu kwa makampuni kuhusina na hii biashara mtandaoni.

Kwa kipindi cha sasa ni vigumu kuepeuka matumizi ya mtandao katika shughuli za kila siku. Biashara mtandaoni sasa imekuwa ikiwanufaisha watu wengi sana.

Unaweza ukawa na mawazo ya biashara na usijue unawezaje kufanya biashara mtandaoni. Deep media wanaweza kukusaidia kuendesha biashara yako kwa njia ya mtandao lakini pia kukutengenezea njia zuri za kibiashara. Tufuate kupitia mitandao yetu ya kijamii hapo chini