Mitandao ya kijamii ni mojawapo ya njia bora ya kukuza chapa yako ya biashara lakini hata maudhui unayoyatengeneza. Lakini kuna jambo unapaswa kulizingatia. Haupaswi tu kuchapisha maudhui kwenye mitandao ya kijamii muda wowote unaotaka. Haupaswi kuchapisha maudhui tu kwa sababu umejisikia kufanya hivyo kwa muda huo. Kuna muda ambao ni bora zaidi kuliko muda mwingine.

Je, unadhani ni muda gani bora zaidi kuchapisha maudhui mtandaoni (posting)?

Kwa bahati mbaya, hakuna jibu lililokamili haswa kujibu swali hili.Ukizingatia kila mtu ana wakati wake wa kupitia maudhui ya mitandaoni. Kila mtu ana wakati wake wa kushinda kwenye mitandao ya kijamii. Lakini pia inategemea na mtandao upi ambao watu hutumia kw asana kwa wakati Fulani.

Kiujumla kuchapisha maudhui mtandaoni (posting) inategemea mambo makuu 3.

  • Walengwa (Targeted audiences)
  • Eneo husika (Region)
  • Muda wa maeneo husika (Time zone)

SOMA ZAIDI:

Hata hivyo, kuna takwimu kubwa zinazoonyesha wakati mzuri hasa wa kuchapisha maudhui kwenye mitandao kama vile Instagram, Facebook, Twitter, LinkedIn pamoja na Pinterest.

  1. Mtandao wa Instagram

Kwa wastani, inatajwa kuwa ni vyema kuchapisha maudhui kwenye mtandao wa Instagram kuanzia majira ya saa 7 mchana hadi saa 11 jioni. Hiki ni kipindi hasa chenye manufaa kwakuwa saa 7 ndio watu wengi uenda kupata chakula cha mchana. Lakini pia muda huo ndio watu upata mapumziko na kuweza kupitia kwenye mitanao yao. Saa 11 kwa kawaida ndi muda wa kumaliza kwa shughuli za kila siku kwa watu wengi.

Lakini pia inatwaja kuwa siku nzuri ya kuchapisha maudhui kwenye mtandao wa Instagram ni Ijumaa.

  1. Mtandao wa Facebook

Watu wengi huingia kwenye mtandao wa Facebook kupitia kompyuta pamoja na simu zao wakiwa kazini n ahata nyumbani. Jinsi gani inatumika mitandao hiyo inategemea na watumiaji.

  • Kwa wastani muda ulio bora kwa ajili ya kuchapisha maudhui kwenye mtandao wa Facebook ni saa 3 asubuhi. Huu ni wakati ambao watu wengi wanaanza kazi na ndio wanaopoingia mtandaoni kwa mara ya kwanza.
  • Mtandao wa Facebook unaonyesha kuwa kuna ongezeko kuwa la watu wanaotumia Facebook kuanzia saa 5 asubuhi mpaka saa 6 mchana wakati watu wakijiandaa kupata chakula cha mchana.
  • Lakini pia kwa B2B, B2C pamoja na software inaonyesha kuwa Saa 9 mpaka saa 10 jioni ni muda mzuri wa kuchapisha maudhui.
  • Siku ya Alhamisi hadi Jumapili inatajwa kuwa ndio siku bora kwa kuchapisha maudhui kwenye mtandao wa Facebook.
  1. Mtandao wa Twitter

Kama ilivyo kwa Facebook, watu wengi hutumia mtandao wa Twitter kupitia simu pamoja na Kompyuta wakiwa kazini n ahata nyumbani.Jinsi inavyotumika inategemea na watumiaji wenyewe.

  • Inatajwa kuwa muda mzuri wa kuchapisha maudhui kwenye Twitter ni kuanzia saa 2 mpaka saa 4 ausubuhi lakini pia saa 6 mpaka saa 9 jioni.
  • Lakini pia kama lengo lako kubwa ni kuongeza retweets basi lenga hasa majira ya mchana au jioni kuanzia saa 11 hadi saa 12.

Zingatia kuwa licha ya kuwa kila mtandao wa kijamii unakupa engagement yake kubwa pamoja na idadi ya wanaotembelea post zako katika saa na siku za wiki. Kiasi cha engagement uchaopata kinategemea na maudhui uliyochapisha kwa walaji wako.

Karibu Deep Media Digital Agency tutakushauri jinsi ya kuweza kutumia mitandao ya kijamii pamoja na platform nyingine ili kuweza kukua kibiashara.