Mwaka 2018, utafiti uliofanywa na Kikundi cha Utafiti cha Leichtman uligundua kuwa 78% ya watu majumbani bado wanatazama Televisheni ya asili au TV ya kebo.

Kwa kuangalia takwimu hiyo, hautaweza kufikiria kuwa utazamaji wa Runinga umepungua. Lakini uhalisia ni kuwa umepungua na hata utazamaji wa matangazo yake.

Kwa mfano, ukizingatia utafiti uliofanywa na nkundi hilo hilo la utafiti kwa 2018, utaona 69% ya nyumba nyingi nchini Marekani wameunganishwa na huduma ya video streaming. Hii ni kutoka 52% kwa mwaka 2016.

Licha ya hayo, utumiaji wa mtandao pia umeongezeka kwa zaidi ya watumiaji bilioni nne tangu mwaka jana. Idadi hiyo inajumuisha zaidi ya nusu ya idadi ya watu wote Duniani, huku Uchina, India na Marekani zikiwa mbele ya nchi nyingine zote kwa watumiaji wa mtandao.

SOMA ZAIDI:

Kuanguka kwa Matangazo ya Televisheni

Kiuhalisia kutokana na idadi kubwa ya watumiaji wa mtandao hii inafanya watu wengi sasa kuanza kuvutiwa na njia ya kigitali kama sehmu ya kuimarisha biashara zao. Zipo sababu nyingi kama vile,

1. Gharama ndogo ya kuendesha matangazo kupitia mtandao

Ni wazi kuwa haihitaji kuwa na bajeti kubwa sana kwa ajili ya kuendesha matangazo ya mtandaoni, ukilinganisha nay ale ya TV. Wafanyabiashara wengi sasa wamwekuwa wakilalamika kukosa bajeti ya kutosha kuendesha matangazo ya biashara au kampuni zao.

Hivyo basi kutokana na kutokuwa na bajeti ya kutosha wengi uamua kutumia njia ya mtandao ambayo pia inaweza kuwafikia watu wengi tena kwa haraka.

2. Matangazo kwa njia ya kidigitali huwafikia walengwa moja kwa moja

Tofauti na matangazo ya Televisheni. Matangazo ya kidigitali huwafikia walengwa kutokana na uwezo wake wa kuruhusu kuwafikia wale tu walaji wa bidhaa au huduma husika. Kwa TV ni tofauti ambapo mtu yeyote yule anayewasha TV kwa madhumuni ya kuangalia kipindi Fulani anaweza kuona hata kama asiwe mlengwa.

3. Matangazo ya digitali ni rahisi kufanya analytics

Ni rahisi mno kufanya uchambuzi wa idadi ya watu waliofanikiwa kuona tangazo la mtandao tofauti na matangazo ya kwenye Televisheni. Hii itakupa muongozo wa kuelewa kwa kiasi gani tangazo lako limetazamwa na wateja wako.

Ni wazi zipo sababu nyingi zinazofanya sasa watu wengi kuamini matangazo kwa njia ya digitali ukilinganisha nay ale ya TV. Deep Media digital agency imewasaidia wengi kwenye upande huo wa matangazo kwa njia ya kiditali. Tafadhali ili kuweza kuunganishwa na mfumo huo wa kidigitali bonyeza HAPA kwa mawasiliano.