Biashara au huduma yeyote inahitaji matangazo. Matangazo haya yanaweza kufanywa kwa namna tofauti kutokana na aina ya biashara/huduma yenyewe au hata eneo husika la biashara. Wapo wanaotumia televisheni, radio, magazeti, majarida mbalimbali kama njia ya kutengeneza mauzo.

Katika kipindi hiki cha sasa sehemu kubwa ya utafutaji wa masoko ya biashara ufanyika mtandaoni. Mara nyingi watu wa masoko hufanya kampeni mbalimbali kwenye mitandao kwa ajili ya kuongeza mauzo.

James, ni mtaalamu wa masuala ya masoko, na amefanya kazi hiyo kwenye kampuni mbalimbali, ndogo na kubwa. Changamoto kubwa ambayo James amekutana nayo, ni kuwa mara nyingi anaajiriwa kwenye kampuni kwakuwa idara ya masoko iliyokuwepo imeshindwa kufanya vizuri.

Kwanini kampeni nyingi za masoko na mauzo zinafeli ndani ya miezi 3 tu?

Zipo sababu nyingi sana zinazosababisha kufeli kwa kampeni nyingi za mauzo. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na,

  1. Kampeni nyingi zinalenga kuongeza idadi ya watu (traffic) badala ya wateja (conversion)
  2. Kufanya sawa na mshindani wako kibiashara (Copying your competitors)
  3. Kuweka bajeti iliyo chini ya kiwango
  4. Kukosa uangalizi thabiti (monitoring)
  5. Kutoongeza bajeti ya kampeni kadri inavyoongeza mapato. (You are not maximizing your profit.

Kiujumla suala la kampeni za mauzo linahitaji uangalizi mkubwa, malengo, bajeti yenye kujitosheleza kulinga na malengo ya kampeni. Deep Media Digital agency chini ya timu yenye uweledi imekuwa ikifanya utafiti kila wakati kuhusiana na mipango thabiti ya kuandaa kampeni mbalimbali za masoko/mauzo. Tembelea kurasa zetu mbalimbali za mitandao ya kijamii pamoja na tovuti yetu.