Ikiwa biashara yako au huduma unayotoa ina eneo rasmi/halisi, basi moja ya mambo ambayo unahitaji kuyafanya ili kukuza biashara yako ni kutumia “Google Map” kwa jina lingine ni “Google my Business” “Google Location”

Huduma hii itakuwezesha kuorodheshwa kwa biashara, huduma au kampuni yako kwenye “Google Map”. Ambapo itakuwa rahisi kwa mteja wa biashara au huduma yako kukufikia kwa haraka.

Kwa kutumia “Google Map” au “Google Location” inatoa urahisi kwa wateja wako kukupata kupitia google na hata kukufikia kwa urahisi sana kwenye biashara au kampuni yako. Unachopaswa kufanya ni kuisajili biashara yako kwenye huduma hii.

Faida za kujisajili na huduma ya “Google Map”/Google My business

Kuna faida nyingi sana na za msingi hasa kwenye biashara au kampuni yako katika kutumia huduma hii. Wengi waliotumia huduma hii wameona mafanikio yake katika kukuza biashara. Faida ni kama zifuatazo,

  1. Inakuonyesha Mwenendo mzima wa biashara yako (General Performance)

Licha ya kuonyesha mahali biashara yako ilipo, pia huduma hii itakuonyesha utendaji na mwenendo mzima wa biashara yako kupitia takwimu za watu wanaoitafuta biashara yako kupitia Google.

Hii itajumuisha vipengele kadha wa kadha vinavyokupa uchanganuzi wa mwenendo mzima wa biashara yako. Vipengele hivyo ni kama vifuatavyo.

(a) Kutambua wateja wako wanaipataje biashara yako kwenye google?

Hapa utaweza kujua wateja wa aina tatu ambao wanaweza kuwa ndio hasa walengwa wa biashara yako, wapo wale ambao wanakutafuta kwa kuandika jina la biashara yako kwenye google, kuna wanaokupata kwa kutafuta aina ya bidhaa au biashara kama ya kwako, na wale wanakupata kupitia jina lako la biashara (branded).

 

(b) Utakuwa na uwezo wa kutambua wapi wateja wanakutafuta kwenye biashara yako.

Hii inaweza kuwa wanakutafuta kupitia ramani au kupitia google moja kwa moja.

(c) Kutambua hatua alizochukua mteja wako baada ya kukupata kupitia google.

Baaada ya mteja kukupata kupitia google anaweza kufanya maamuzi kuhusiana na biashara yako. Maamuzi haya yanaweza kuwa,

  • Kupiga simu
  • Kuomba ramani ya kukufikia kwenye biashara yako
  • Kutembelea kwenye tovuti yako ambayo umeweka kwenye huduma hii.

(d) Itakusaidia pia kujua ni muda gani wateja huwa wanatembelea biashara yako.

Kupitia Google My business unaweza kutambua ni muda upi wa kibiashara kwako. Unaweza kuona muda gani ambao wateja huwa wanaitafuta sana biashara yako kupitia google.

(e) Lakini pia itakusaidia kufanya mawasiliano moja kwa moja na wateja wako

Kupitia ujumbe ambao wanaouacha kwenye ukurasa wako, unaweza kufanya majadiliano na mteja ili uweze kujua ni wapi unapaswa kuboresha biashara yako ili uweze kukuza mauzo. 

(f) Lakini pia unaweza kuweka picha za bidhaa zako ili wateja wako waweze kuona kile ulicho kuwa nacho.

Hii inamaana kuwa inakupa fursa si tu ya kumuonyesha mteja wapi biashara yako ilipo, bali inakupa pia fursa ya kumuonyesha mteja baadhi ya bidhaa ulizonazo. Lakini pia hii itakusaidia kuona idadi ya watu wanaoangalia bidhaa zako.

Kiujumla dhana ya kuweka “Location” ya biashara yako inajumuisha vitu vingi si tu kuweka ramani ya biashara na kubaki hivyo. Inajumuisha uchambuzi wa takwimu na maoni ya wateja wako ili kuendelea kuwa na mwenendo mzuri wa biashara yako.

Karibu Deep Media Digital Agency tukusaidie sio tu biashara yako kuoneka ilipo bali pia kukufanya uwe karibu na wateja wako ikiwa ni pamoja na kujua mahitaji yao kwa wakti.