Ukiwa na biashara yenye physical location (Ofisi) ambapo wateja wanaweza kukutembelea basi makala hii ni kwaajili yako, kwasababu ndani yake utapata kuona vidokezo vya namna unavyoweza kuiweka biashara yako iweze kuonekana kwenye google search.
Hasa utapata kuona umuhimu wa kuiweka biashara yako iwe inapatikana kupitia google search.

Google search imekuwa sehemu pendwa sana ambapo watu wengi sasa hutumia kwa ajili ya kutafuta taarifa kuhusu biashara, bidhaa flani au kujua wapi huduma mbalimbali zinapatikana.
Tumia nafasi hiyo kujiongezea wateja kwa kuhakikisha unapatikana kwenye google search. Hivyo basi kama bado hujaiweka biashara yako iweze kutambulika kupitia google search, wakati ni huu. Na kupitia makala hii utaona faida kuu kwanini ufanya hivyo

Google Local SEO ni mchakato wa kuirodhesha biashara/kampuni yako kwenye Google na Google Maps ili watu/wateja wanapokutafuta waweze kukupata, kuwasiliana na kukufikia kwa urahisi.

Local SEO Tanzania

SOMA ZAIDI

Faida za Google Local SEO kwenye biashara yako.

  1. Kukua/kutanuka kwa biashara yako

Tovuti yako ni sehemu ya pili inayokuwakilisha wewe kwenye soko la biashara yako. Kwa msaada wa SEO, unaweza kufikia wateja wako kwa urahisi sana na kuwasaidia kutambua aina gani ya biashara unayoendesha, huduma gani unazozitoa, na mengi zaidi. Hii husaidia katika kujenga upanuzi wa Biashara kupitia wateja na vitengo vya biashara.

  1. Uelewa miongoni mwa Wateja wako

Lengo kuu la Local SEO ni kujenga uelewa katika soko kuhusu uwepo wako ili watu ambao wanavutiwa na huduma zako wajaribu kuwasiliana nawe kupitia google (Local SEO)

Mfano, uchambuzi wa kampuni moja umeonyesha namna wateja wao wanavyowatafuta kupitia Google search, kuwa idadi wa watu waliotafuta huduma au taarifa za kampuni kupitia Google Search Local SEO walikuwa 181. Kati yao

  • Waliotafuta kwa kuandika jina la kampuni moja kwa moja kupitia google walikuwa 136
  • Waliowatafuta kwa kuandika jina la huduma wanazotoa walikuwa 44
  • Waliotafuta kampuni kwa kuangalia biashara zinazofanana alikuwa 1
  • Waliofanya maamuzi ya kutafuta taarifa zaidi walikuwa 5
  • Kati yao 1 alitafuta ramani ya kufika ofisini moja kwa moja na alifanikiwa kufika
  • Kati yao 3 walitembelea moja kwenye tovuti ya kampuni
  • Na 1 kati yao alifanya maamuzi ya kupiga simu

  1. Itakusaidia kuongeza Mapato kwenye biashara yako

Unapoiweka biashara yako juu kwenye Google Search unafanya watu wakufikie kwa urahisi zaidi. Ukiweza kufikiwa na watu wengi kwa urahisi unatengeneza mtandao mkubwa wa wateja ambao ndio chanzo chako kikuu cha kuongeza mapato kwenye biashara yako.

  1. Inasaidia kujenga uaminifu kwa wateja wapya.

Kupitia “Google review” ambapo mara mtu/mteja anapotafuta jina la kampuni au huduma anaweza kuona mapitio na maoni ya wateja mbalimbali ambao walitafuta jina la kampuni au huduma na baadaye kuacha maoni yao kwa kuipa nyota.

5. Kuongeza Trafiki kwenye Tovuti.

Unapokuwa umeiorodhesha biashara yako kwenye Google search inamaana unataka ionekane na watu wengi tena kwa urahisi na haraka. Hivyo basi Local SEO inaweza kukuongezea trafiki kubwa ya wateja wanaotembelea tovuti yako mara kwa mara kwasababu punde tu mteja atakapo kutafuta kupitia google, ataona taarifa za website yako na kuitembelea.

Biashara na makampuni mengi sasa yamekuwa yakipigana kwenye soko la ushindani kwa kuzitambulisha biashara zao au huduma zao kwa watu Zaidi. Njia ya Google Local SEO imekuwa njia mbadala wa wafanyabiashara wengi ili kuweza kurank biashara zao kwenye mtandao. Unasubiri nini sasa na wewe kuanza kuitambulisha kwa urahisi biashara au kampuni yako kwa wateja wako.

Baadhi ya taarifa za biashara yako zinazoweza kupatikana kirahisi kupitia google search

  • Anuani ya biashara kwenye google maps
  • Mida yako ya kazi
  • Namba za simu za mawasiliano za ofisini kwako
  • Tovuti ya biashara yako
  • Picha za matukio ukiwa ofisini, kazini na ukiwa unahudumia wateja wako.

Hii ni njia muhimu sana ambayo hutumiwa na biashara nyingi kwa ajili ya kuzifanya biashara zao au kampuni zao kutambulika kwa haraka Zaidi na wateja wake. Hakikisha wateja wako wana uwezo wa kuwasiliana na wewe na kukufikia kirahisi kupitia Google search.

Je umeorodhesha biashara yako kwenye Google Search na kwenye google maps?
Karibu Deep Media tukuhudumie.
Bonyeza HAPA kwa mawasiliano zaidi.