Watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mengi kuhusiana na namna ya kuingiza kipato kupitia Youtube. Baadhi ya maswali hayo ni pamoja na,

  • Je, ni kweli unaweza kuingiza fedha kupitia Youtube?
  • Nini unapaswa kufanya ili kufanikiwa kupata fedha?
  • Muda gani unachukua kuweza kuipata fedha hiyo?
  • Na, je, unawezaje kuipata fedha hiyo moja kwa moja?

Kwanza nipende kusema tu kuwa ni kweli unaweza kupata au kuingiza kipato kupitia Youtube. Jambo la msingi ni kufuata misingi na kanuni iliyowekwa ili uweze kufikia malengo.

Yapo mambo kadhaa unayopaswa kuyafanya kabla ya kufikia hatua ya kupata fedha au kulipwa kupitia Youtube. Kwanza unatakiwa kufahamu sio tu kumiliki youtube kunaweza kukupatia fedha, la asha, unapaswa kuchapisha maudhui (Content) kwenye youtube kwa ajili ya kuweza kuifanya akaunti ya youtube kuingia kwenye mchakato wa kibiashara. Yapo mambo kadhaa ya kufuata,

Masharti ya kufuata

  1. Unapaswa kufungua Channel ya Youtube (Youtube Channel)
  2. Channel lazime ithibitishwe, inaamana kuwa Youtube akaunti yako lazima iwe imethibitishwa (Verified account)
  3. Kuwa na Maudhui (content)
  4. Maudhui yafuate Misingi na matakwa ya Google/Youtube (Soma matakwa HAPA)
  5. Lazima uwe na Subscribers 1000 pamoja na masaa 4000 ya kutazamwa kwa maudhui yako (watching time) ili uweze kuingia kwenye mfumo wa kifedha (Monetization). Na hii ni ndani ya miezi 12.
  6. Lazima ufungue akaunti ya Google Adsense. Hii ndio inayoratibu mfumo mzima wa malipo ya kazi yako. Hapa ndipo uatakapochagua mfumo wa kupokea pesa na ndipo utakapata PIN yako ya kuratibu malipo ya fedha zako.

Kumbuka:

Ili kufungua akaunti ya Google Adsense unapaswa kuwa na vigezo vyote hapo juu. Lakini pia google Adsense inakutaka lazima uwe umefikia kiwango cha dola 100 ili uweze kukubaliwa kuanzisha huduma ya malipo.

Tambua hayo yote yanahitaji mfumo au mlolongo wa muda. Wapo wanaodhani kuwa ukifungua akaunti leo basi kuanzia kesho utalipwa. La asha. Hii ni process ndefu, ila jambo la msingi timiza kwanza matakwa ya Youtube account/channel kabla ya kuwaza fedha. Kwa maswali na taarifa zaidi tutembelee Deep Media Digital Agency tutembelee kupitia akaunti zetu za Mitandao kijamii

Instagram: @deepmediatz

Twitter: @DeepMediaTz