Tovuti Mpya

Kwa namna ambavyo technologia inakuwa kwa kasi, ni muda sahihi kwa wewe kuhamia katika mfumo wa kidigitali ili kuweza kukuza Biashara yako kwa kutengeneza tovuti inayolipa. Ni lazima kufikiria kuwekeza katika tovuti mpya ambayo ni;

  • Rafiki kwa mtembeleaji au mtumiaji
  • Tangamanifu na simu(mobile Responsive)
  • Imetumia technolojia ya kisasa za utengenezaji tovuti
  • Inakidhi mahitaji yako ya Biashara

Tovuti inabeba taswira ya biashara yako au ya kampuni yako popote ulimwenguni. Hivyo ikiwa hutozingatia Utengenezaji bora na sahihi wa tovuti, basi Utaharibu taswira ya bishara yako na kampuni yako.

Kuwekeza katika tovuti mpya haimaanishi yakwamba ubadilishe kila kitu katika tovuti uliyonayo. Ila unaweza badilisha baadhi ya vitu vitakavyopelekea Biashara yako kuendelea kukua kwa kasi.

Swali la kujiuliza ni vitu gani utavikosa/Au ni gharama gani unaipata  usipowekeza katika tovuti mpya?

Tovuti Mpya

Kukusaidia kuweza kufanya maamuzi kama huu muda ni sahihi kwako kutengeneza tovuti mpya, tumekuorozeshea sababu 5 za kwanini uwekeze katika  kutengeneza tovuti;

  1. Kukosekana kwa  ubora, Ubunifu na ushawishi katika Makala.

Makala ni muhimu sana pale linapokuja suala la kukuza Jina lako na Biashara yako. Madhumuni bora na zenye ushawishi zinatumika kuwabadilisha wale watu wanaotembelea katika tovuti yako Kuwa Leads na hata kuwa wateja wa Bidhaa au Huduma Unazozitoa.

Pale unapoweka Makala Bora katika tovuti au blog yako utawavutia watu wengi kuweza kutembelea Ukurasa wako. Bila kuwa na makala bora na zenye ubunifu kila wakati, utakuwa huna jipya na wateja wenye uwezo watapoteza mvuto na biashara yako.

READ MORE: ONGEZA KIPATO ZAIDI

  1. Muundo mbaya wa Tovuti

Kosa hili hufanywa na watu wengi sana kutokana na maarifa duni ya usanifu Mtandao. Ni muhimu kuhakikisha tovuti yako inasomeka vizuri na kuvutia.

  1. Kasi ndogo ya kufunguka

Matumizi ya Technolojia ya zamani au hata kuweka mambo mengi kupita kiasi katika ukurasa mmoja kunafanya tovuti kuwa na kasi ndogo ya kufunguka. Kero hii inawafanya watu wengi wasifungue tovuti yako kwasababu inawapotezea muda wao mwingi.

Tovuti Mpya

  1. Haija tumia technolojia ya kisasa na Haitangamani na Simu(Outdated and not Mobile responsive)

Hakikisha unawekeza kwenye teknolojia ya kisasa ili tovuti yako iweze kukidhi mahitaji muhimu ya watumiaji. Mfano ni lazima tovuti yako ipatikane vizuri kwenye simu, tablet na aina mbali za computer pamoja na browser tofauti. Ukiwa na tovuti ambayo ina muonekano tofauti tofauti kwenye kila browser au kwenye  kila aina ya computer au simu inakera wateja na kuwafanya wasiendeleee kuitumia au kuitembelea tovuti yako

  1. Tovuti Haija unganishwa na mitandao ya kijamii

Mitandao ya kijamii ni mifumo maalumu unaowasaidia au kuwawezesha watumiaji wake kuwasiliana na kutumiana taarifa kwa njia ya meseji, Sauti (audio) na picha za mnato au mtikisiko (video)

Mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook, Youtube, LinkedIn, Instagram n.k ni moja ya Mifumo Mizuri Ya kutafuta Masoko katika Biashara yako. Kuna mitandao Mingi sana ambayo unaweza kukuza na kuongeza Uwepo wako katika Mitandao hiyo ndani ya Tovuti Yako. Ni muhiumu sana tovuti yako iwe na mahusiano ya moja kwa moja na mitandao ya kijamiii. Ikiwa na maana kwamba watu wanakutembelea kwenye mitandao ya kijamii ni muhimu waweze kuelekezwa kwenye tovuti yako.

 

 

Tovuti Mpya

 

  1. Hairuhusu wateja au watembeleaji kufanya maamuzi(Call To Action)

Tovuti inatakiwa kuwa ni sehemu ya wateja au watembeleaji kuweza kufanya maamuzi. Kwa mfano kama watembeleaji watakuwa wanatafuta ni namna gani wanaweza kuwasilliana na wewe, basi tovuti hiyo inakuwa imepoteza lengo. Namba za simu, barua pepe na wapi unapatikana au kitufe kitakachoonyesha maelezo zaidi ya namna gani unapatikani ni muhimu sana kuwako katika tovuti yako.

Mwisho

Kutengeneza tovuti ya namna hii au kubadilisha iliyopo iweze kufanya Vitu vilivyoainishwa hapo juu ni matokeo yamabadiliko katika Soko la Biashara. Kama Tovuti yako haiendani na  na Biashara yako au watu unaotamani kuwafikia ni wakati wa kutengeneza Tovuti mpya. Zingatia kuwasiliana na Kampuni Kama Deep Media Yenye Uzoefu na Ubobevu wa miaka mingi wakutengeneza Tovuti Inayokulipa.