Tovuti ni muhimu sana unapotaka kuanzisha biashara yako lakini sio kila tovuti inaweza kuwa bora kwa biashara yako. Wavuti bora itakufanya iweze kumshawishi mteja awe na uhuru wa kuitembelea kila wakati anapohitaji bidhaa au huduma yako.

Ili kuifanya biashara au kampuni yako ikue kwa haraka ni wazi matumizi ya wavuti ni vigumu kuyaepuka. Kitu kikubwa cha kuzingatia ni kuwa tovuti yeyote ya biashara inahitaji kukidhi mahitaji ya biashara au huduma unayoitoa kwenye kampuni yako.

Vitu 5 vya kuzingatia unapohitaji tovuti ya kibiashara.

  1. Usalama wa wavuti yako (Security)

Kutokana na kukua kwa teknolojia kwa kasi hatari ya uwepo wa watu wenye uwezo wa kuingilia wavuti yako ni kubwa mno. Hakiksha wavuti yako inakuwa salama muda wote kwa kuwekewa viambata vyenye kuilinda wavuti yako. Yeyote atakyehusika na utengenezaji wa wavuti basi anapaswa kuangalia suala la usalama wake.

Tovuti zote zenye kurasimisha malipo ya mtandaoni ni muhimu sana kuzilinda kwa ufanisi zaidi ili kuweza kulinda taarifa za mteja wako.

SOMA ZAIDI:

  1. Utendaji kazi (Perfomance)

Unapokuwa unatafuta taarifa zozote muhimu mtandao hakuna kitu kinachosha kama ukurasa kufungua taratibu. Hakiksha tovuti yako ina uwezo wa kufunguka kwa haraka zaidi ili kumpa urahisi mteja wako kuendelea na huduma.

Matatizo ya ukurasa  kufunguka kwa taratibu yanaweza sababishwa na vitu vingi sana. Vitu kama matumizi ya picha kubwa (zenye Mb kubwa), mpangilio wa mwonekano wa wavuti  (lay-out) na hata viambata vyake (plug-ins).

  1. Uwepo wa hewani (Uptime)

Lazima uwe na uhakika kuwa ukurasa  wako unapatikana hewani muda wote. Suala la biashara linahitaji uhakika wa jambo. Mteja anapokuja kwenye ukurasa wako basi awe na uhakika kuwa anaweza kukufikia kwa muda husika. Hakikisha tovuti yako inafikika kwa haraka zaidi.

Mara nyingi matatizo ya ukurasa kutofikika kwa urahisi usabibwa na kutozingatia taratibu. Muda mwingine mmiliki huwa anahitaji wavuti ambayo itakuwa ya bei rahisi sana.

  1. Wavuti yenye kuingilika kwenye kivinjari (browser) tofautitofauti.

Hakika tovuti yako inaweza kuingilika kwa kutumia kivinjari chochote tena bila ugumu wowote. Hii itasaidi kumpa urahisi mteja wako wa kuweza kupa huduma zako kwa urahisi.

 

  1. Yenye kuweza kuingiliana na mitandao ya kijamii

Unahitaji mitandao ya kijamii kama instagram, facebook na hata twitter ili kudumisha biashara yako. Hakikisha tovuti unayohitaji kwa biashara yako ina uwezo wa kuunganishwa na mitandao yako ya kijamii kwa urahisi.

  1. Kuchagua jina la wavuti na muendeshaji

jina zuri la watuvi yako linatoa ujumbe mkubwa biashara yako. Kuwa makini kwenye kutengeneza jina la wavuti yako ambalo ndio jicho la biashara yako. Mteja anapoingia kwenye injini pekuzi basi haraka awe na uwezo wa kukupata. Hakikisha pia mtu anayeendesha tovuti yako ana uwezo wa kuiendesha kwa ustadi zaidi.

Vipaumbele vyote hivyo ni muhimu kwa ajili ya kutengeneza msongamano kwenye wavuti yako. Hii itakusaidia kupata wateja wengi kwenye biashara kupitia tovuti yako.

Kwa msaada zaidi ili kuweza kufahamu au kupata ushauri kutoka wataalam BONYEZA HAPA. Watakushauri na kukupa njia bora za kukuza biashara yako.