Unajua kuwa zaidi ya 78% ya biashara nyingi kwa sasa zimejikita kwenye mitandao ya kijamii? Asilimia hii ni kubwa zaidi ukilinganisha na miaka mitano iliyopita. Kampeni za mauzo mbalimbali zainazofanywa kupitia mitandao ya kijamii zinaonyesha kuzaa matunda zaidi kuliko zile za namna nyingine. Na hii imekuwa ndio chachu hasa kwa wafanyabiashara kutumia kama njia ya kuongeza mauzo.

Kampuni moja ya usamabazaji wa vifaa mbalimbali maarufu kama “Distributor” katika utafiti wake wameonyesha kuwa kuna utaofauti mkubwa wa mauzo hasa pale wanapoamua kutumia kampeni za mauzo kwenye mitandao ya kijamii. Kwa wao kampeni za mauzo kwenye mitandao ya kijamii zinawaongezea mauzo kwa zaidi ya 50%

Nguvu ya kampeni za mauzo kupitia mitandao ya kijamii

Mfumo wa kibiashara sasa unabadilika kwa kasi, ni wazi hata watu wa masoko nao wanajaribu kuendana na mfumo mpya wa uuzaji na ununuzi wa bidhaaa/huduma. Hakuna shaka kwenye zama hizi za kisasa kuona kuwa sehemu kubwa ya mikakati ya masoko ni matumizi ya mfumo wa kidigitali.

Kukiwa na zaidi ya watumiaji bilioni 2.4 wa facebook kila mwezi. Lakini pia zaidi ya watumiaji bilioni 1 wa Instagram kila mwezi, unawezaje kuiacha fursa hii na kuigeuza kuwa fedha?

Kwa kupitia kampenzi za mauzo za mitandao ya kijamii utaweza, kutengeneza wateja watakaoendana na matakwa ya biashara yako, kwakuwa itazingatia,

-Umri wa wateja unaowalenga

-Shughuli za wateja walengwa

-Jinsia

-Kipato

-Sehemu/mahali

-Wateja wenye kupendelea bidhaa yako (Interest).

Kwa kutumia taarifa hizo ni wazi unaweza kuwafikia wateja wengi kwa muda mfupi tena wale ambao umewakusudia katika bisahara yako.

Deep Media Digital Agency kwa kipindi cha muda mrefu imekuwa ikiendesha kampeni mbalimbali za mauzo kupitia mitandao ya kijamii. Kampeni hizi kwa asilimia kubwa zimekuwa zikizaa matunda n ahata kuwavutia wafanyabiashara wengine.

Unasubiri nini sasa na wewe kuunganishwa kwenye kampeni hizi zinazofanywa kwa weledi mkubwa na matokeo yake makubwa. Tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Instagram, twitter pamoja na Facebook, kwa mawasiliano zaidi Bonyeza HAPA