Kutokana na jinsi gani watu wanaweza kuifikia huduma ya mdahalisi (Internet) kwa sasa. Je, unaweza kuamini nikisema kuwa idadi ya watu wanaoingia mtandaoni kila siku inaongezeka?

Ni ukweli. Uhalisia uko hivi, watumiaji wa mtandao miongoni mwa walio watu wazima idadi yao imeongezeka kwa 5% na hii ni kwa miaka 3 iliyopita kulingana na utafiti uliofanywa na taasisi ya kitafiti ya Pew Research.

Ijapokuwa tunazungumza lugha hii kila wakati. Lakini uhalisia ni kuwa hata namna ya watu wanavyofanya manunuzi ya bidhaa zao ulimwenguni imebadilika. Hii inamaanisha kuwa huduma ya masoko kwa njia ya kawaida inaonekana kutokuwa na athari chanya kwa sasa kama ilivyokuwa awali.

Kutokana na mageuzi makubwa ya teknolojia mpya ulimwenguni. Biashara nyingi, ndogo, za kati na hata kubwa zinajitahidi kufanya kila kitu kinachowezekana kuziendeleza ili kuendana na jamii ya sasa.

Huduma ya masoko ni jambo la kukuunganisha mfanyabisahara na mteja wako katika muda muafaka na sehemu sahihi. Ikiwa na maana kwa sasa unapaswa kukutana na mteja wako popote alipo na kwa wakati sahihi kwa sababu tunaamini tayari mteja ametumia muda mrefu kuwa mtandaoni kwa ajili ya kupata huduma au bidhaa.

SOMA ZAIDI:

Nini maana ya Masoko  Mtandaoni (Digital Marketing) ?

Masoko Mtandaoni (Digital Marketing) ni utafutaji wa masoko ya bidhaa au huduma kwa kutumia teknolojia ya kidigitali zaidi kupitia  njia ya mdahalisi (internet) lakini pia ikijumuishwa na simu za mkononi, matangazo ya kuonekana (display advertising) na njia mbalimbali za kidigitali.

Ni matumizi ya mbinu za mbalimbali za kidigitali na njia za kumuunganisha mteja ambaye hutumia muda mwingi akiwa mtandaoni.

Maendeleo ya mfumo huu wa kibiashara yalianza kujitokeza kwenye kipindi cha miaka ya 1990 na 2000 na kubadilisha mfumo mzima kutangaza biashara kupitia njia mpya ya kiteknolojia.

Mbinu za Masoko Mtandaoni (Digital Marketing tactics)

Meneja masoko bora daima huwa ana picha halisi ya jinsi kila kampeni yeyote ya masoko inayosaidia kufikia malengo ya kampuni. Na kwa kutegemea na malengo ya mkakati wake wa masoko anaweza kusaidia kampeni kubwa kupitia njia za bure na za kulipwa zilizopo.

Anaweza kutumia njia ya kuandaa maudhui kwa ajili ya blogu amabyo yanaweza kutengeneza wafuasi wa kutosha. Kutumia mitandao ya kijamii kutangaza maudhui ya blogu ya biashara husika na hata matumizi ya barua  pepe za kimasoko (Email Marketing).

Hizi ni baadhi tu ya mbinu za masoko mtandao.

  1. Matumizi ya SEO (Search Engine Optimazation) kama mbinu ya kufanya maudhui yako yaonekane juu pamoja nakufikia watu wengi kwa haraka.
  2. Maudhui ya kimasoko (Content Marketing) kwa ajli ya kuwekwa kwenye blogu, vipeperushi vya mtandaoni (Online brochures), n.k.
  3. Matumizi ya mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter, LinkedIn Snapchat, Pinterest pamoja na Google+ katika kutangaza biashara, kukuza jina la biashara (branding & brand awareness) pamoja na kuongeza wateja kwa wingi.
  4. Matumizi ya Pay-Per-Click (PPC) kama njia ya kuongeza idadi ya watu kwenye wavuti kwa kumlipa mchapishaji (Publisher) kila tangazo lako linavyobonyezwa. Mfano Google AdWords.
  5. Affiliate Marketing –Kupokea kiasi cha fedha kutokana na kutangaza biashara ya mtu mwingine.
  6. Native Advertising
  7. Marketing Automation
  8. Barua Pepe za kimasoko (Email marketing)
  9. Inbound Marketing
  10. Matangazo ya mtandaoni (Online PR)

Kwanini utumie Mtandao kutafuta masoko?

  1. Kufikia kimataifa (Global reach).

Kwa kutumia tovuti, itakuwezesha kutafuta masoko mapya nje ya eneo lako la biashara na kujikuta unafanya biashara ndogo tu kimataifa.

  1. Gharama kuwa ndogo lakini inafika katika mawanda mapana.

Kuwa na kampeni ya kimasoko iliyoandaliwa vizuri na kupangiliwa ipasavyo na yenye ufanisi haitakuchukua gharama kubwa kwa ajili ya kuitangaza tena katika mawanda mapana. Tofauti na kama ukiamua kutumia njia ya kawaida ya kutangaza biasahara kama vile kutumia kwenye runinga, redio na hata magazeti.

  1. Ufuatiliaji na upimaji wa wafuasi wake/wateja

Kupima ufanisi wa njia yako ya masoko mtandaoni ni rahisi sana. Unaweza kutumia njia kama kichanganuzi kupitia wavuti (web analytics) kujua takwimu za wafuasi wako, wateja wako, wamanda ya kampeni yako tofauti na kutumia njia ya kawaidia ni vigumu sana kufanya uchanganuzi. Itakugharimu mud asana kupata taarifa. Lakini pia Web analytics itakusaidia kujua wangapi wanatumia tovuti yako na wangapi wanaitika kwenye matangazo yako lakini pia kiasi gani cha fedha unaweza kuingiza.

  1. Kujitegemea

Ikiwa taarifa za mteja wako zimeunganishwa na tovuti yako basi muda wowote mtu anapotembelea ukurasa unaweza pata taarifa na kupokea ofa.

  1. Uwazi (Openess)

Kwa kutumia mitandao ya kijamii na kuiendesha ipasavyo, unaweza kutengeneza uaminifu kwa mteja wako kwa kuwa umetengeneza sifa kutokana na kuonekana kwa wazi kwa kile unachofanya.

  1. Ushindani

Masoko ya mtandaoni yamekuja kuleta changamoto mpya kati ya biashara ndogo na biashara kubwa. Biasahara ndogo sasa nao wana nafasi ya kuingia kwenye soko la ushindani katika idara ya masoko kwakuwa haihitaji gharama kubwa ambapo awali biashara kubwa walikuwa wanaweza kulipa.

Ni wazi mageuzi haya makubwa yamekuja na changamoto chanya kwa biashara mbali mbali hasa katika kusaidia kukuza na kutangaza biashara kwa ajili ya ustawi ulio bora.

Kwa kuzingatia hilo kampuni ya Deep Media ambayo imekuwa ikifanya utafiti kwa muda mrefu sasa imekuja na ufumbuzi wa jinsi gani biashara zinaweza kufanikiwa  kupitia mfumo wa kidigitali. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa KUBONYEZA HAPA.