Ni wazi mtandao wa facebook unaendelea kutawala katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii.Facebook imekuwa ndio mtandao namba moja ulimwenguni  ambao unawaunganisha marafiki na kubadilishana baadhi mambo na taarifa mbalimbali. Zaidi ya kuwa sehemu ambayo marafiki ukutanja, Facebook imekuwa ukumbi wa kutafuta masoko kwenye biashara mbalimbali kwa sasa.

Deep Media imeandaa Facebook Marketing Webnar  maalumu kuelezea kwanini Facebook itumike kama njia kuu ya kutangaza biashara yako. Namna gani facebook inaweza kukusaidia kuitangaza biashara yako.

SOMA ZAIDI:

Kwanini Facebook itumike kama njia kuu ya kutangaza biashara?

  1. Facebook ina watumiaji zaidi ya billion 2

Facebook ina watumiaji wengi zaidi kuliko mtandao wowote wa kijamii ulimwenguni kote. Mtu ambaye ndio kwanza ameingia kwenye mitandao ya kijamii basi bila shaka anaweza kutumia njia kuitangaza biashara yake.

Takwimu za mitandao ya kijamii maarufu kwa mwaka 2018

Takwimu za mitandao ya kijamii maarufu kwa mwaka 2018

  1. Facebook inamiliki mitandao mingine ya kijamii.

Mtandao wa Facebook, inamiliki mitandao mingine kama Instagram, Facebook Messenger na Whatsapp. Uwepo wa mitandao hiyo yote inakupa urahisi kuunganisha watu wengi kwa wakati mmoja. Mfano unapokuwa kwenye mtandao wa Instagram unapewa uwezo wa kuwaalika rafiki zako wengine kutoka facebook kujiunga na wewe kwenye mtandao wako wa Instagrama hivyo kutengeneza mtandao mkubwa wa marafiki na wateja.

  1. Kila mtumiaji wa Facebook ana marafiki zaidi ya 200

Hii ni muhimu kwa sababu inatengeneza kitu kinaitwa “Viral Effect” mfano umelike page ya mtu halafu una marafiki zako ambao wana interest kama ya kwako moja kwa moja hao marafiki wataona kurasa uliyoipenda na wao wanaoweza kuipenda pia.

Hii itakusaidia katika kusambaza taarifa wa urahisi na kwa haraka.

  1. Facebook inatoa nafasi ya Matangazo yake yenyewe (Facebook Ads./Classic Ads.)

Mtandao wa Facebook unatoa muundo wa matangazo yake yenyewe ambayo yanajitokeza kwenye upande mmoja wa ukurasa wako wa Facebook. Muundo huu wa matangazo unaonekana kuwa bora zaidi katika kutafuta masoko kwa sababu tangazo linaweza kuwafikia watu wengi sana kwa urahisi na haraka.

Ili kuweza kufahamu zaidi ni kwa jinsi gani unaweza kutumia Facebook kama njia kuu ya kutangaza biashara yako tafadhali usikose kufuatilia Webinar ijayo kujua zaidi kuhusu Facebook. Au wasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA.