Je, unajua kuwa zaidi ya watu wapya Milioni moja wanapatikana mtandaoni kila siku? Kwa mujibu wa Ripoti za kitakwimu kuhusiana na idadi ya watu mtandaoni kutoka Hootsuite imeonyesha ripoti hiyo kwa 2019. Ripoti imeonyesha takwimu ya kushangaza katika uchambuzi wa mwenendo wa digitali na matumizi ya mitandao ya kijamii katika nchi na maeneo zaidi ya 230 tofauti.

Kwa biashara za sekta zote. Idadi hii ya watu wapya inayoingia kwenye mtandao kila siku inatoa fursa ya kazi mbalimbali. Fursa kama kutafiti na kununua bidhaa na huduma, hutoa fursa nyingi ambazo haziwezi kupuuzwa.

Uchunguzi umebaini mambo ya kuvutia kutokana na  mwenendo wa sasa wa mtandao na mitandao ya kijamii ambapo biashara ndogo ndogo zinapaswa kuwa na ufahamu wa kuhakikisha kutumia fursa ya kidigitali kwa faida.

SOMA ZAIDI:

Maeneo ya kuzingatia kutengeneza fursa kupitia mtandao.

  1. Mwenendo wa digitali 2019 (Digital Trend 2019)

Angalia baadhi ya dhana muhimu kutoka kwenye ripoti ambapo biashara ndogo ndogo zinapaswa kujua kuhusu na kutekeleza ipasavyo. Mwenendo wa digitali kutokana na ripoti ya Hootsuite ni wazi unaonyesha kuwa na matokeo chanya hasa kwa biashara ndogo ndogo.

  1. 45% huwa wanaingia kwenye kurasa zao pendwa za kijamii

Mitandao ya kijamii inaendelea kuwa muhimili unaoongoza kama uwanja unaotumiwa na watu zaidi ya milioni moja wanaoingia mtandaoni kila siku.

Kulingana na utafiti wa Hootsuite, 45% ya Dunia – karibu watu bilioni 3.5 kwa kila mwaka wanaingia kwenye kurasa zao pendwa za mitandao ya kijamii.

Takwimu zinajionyesha zenyewe, 45% ya watu Duniani, ambao ni karibu watu bilioni 3.5 wanajiunga mara kwa mara kwenye majukwaa (Platforms) yao ya kijamii. Hiyo ni ongezeko la karibu 9% mwaka mzima.

Takwimu zinaonyesha Mtu wa kawaida ana wastani wa akaunti nane za mitandao ya kijamii. Na huku akijihusisha na ujumbe unaokua kwa kasi ya ajabu , amabapo zaidi ya jumbe bilioni 60 hutumwa kupitia WhatsApp peke yake kila siku.

Kwa idadi hii kubwa ya watu wanaotumia kurasa zao za kijamii kila siku, inafanya mitandao ya kijamii kutoa fursa kubwa kwa biashara ndogo kukua  zaidi, kushirikiana na wateja wake ambao ndio walengwa  na hatimaye kuuza bidhaa au huduma zaidi.

  1. Youtube ndio mtandao pekee unatazamwa na zaidi ya 75% ya watu kupitia simu za mkononi.

Takwimu nyingine inayovutia iliyokusanywa kutoka kwenye Ripoti inahusiana na kupanda kwa kasi kwa mahitaji ya maudhui ya video.

Uchunguzi huo uligundua kuwa YouTube ni jukwaa la kijamii linalofanya kazi zaidi nchini Marekani. Aidha, namna ya uangaliaji wa video umebadilika sana ambapo utafiti unaonyesha 75% ya wanaotazama maudhui ya video hutazama kupitia simu zao za mkononi.

Hivyo basi. Kwa biashara ndogo ndogo, kutengeneza maudhui yenye kushirikisha wateja, ya kutangaza biashara au huduma kupitia YouTube, inamaanisha kuwa wanaweza kufikia mamilioni ya watu wanaotazama mtandao wa YouTube kila siku hasa wale wateja wadogo ambao hutumia simu za mkononi kupata maudhui.

 4.     70% ya watumiaji wa internet hutumia jumbe za simu (Mobile Messaging)

Huu ni mwelekeo mwingine muhimu wa digitali ulioonyeshwa katika ripoti ni ambapo  biashara ndogo ndogo zinapaswa kuwa na ufahamu wa takwimu hiyo ili waweze kushugulika nazo. Fikiria ni asilimia 70 ya watumiaji wa intaneti, wote wanatumia ujumbe wa simu. 

Kwa mara moja kuunganishwa na wateja pamaoja na wateja wanaotarajiwa kwa ujumbe wa papo hapo inakuwa njia bora kwa biashara katika kujenga uhusiano mzuri pamoja na kuzalisha wateja ili kukua biashara yako.

Takwimu za Hootsuite ni wazi zinatoa picha ya biashara katika siku za usoni. Kwa idadi hiyo kubwa wa watumiaji wa mtandao (Internet) ni wazi ili biashara kujitanua zaidi hauwezi kuwaepuka.

Ili kuweza kukuunganisha na mamilioni ya watu hao waote ambao hutumia mtando kila siku katika kununua bidha au kupata huduma. Deep Media inakupa fursa kwa ajili ya kukuza biashara au huduma yako. Tafadhali wasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA.