Kuwa na semina ya mtandaoni iliyojaa taarifa za kutosha ni jambo zuri sana kwenye biashara yako. Lakini unajua kipi bora, zaidi ya kuwa na idadi kubwa ya wafuasi kwenye semina yako ya  mtandaoni? Wabadilishe wafuasi wako wawe wateja.

Ufunguo wa kuwabadilisha kundi kubwa la wafuasi wa kwenye semina yako ya mtandaoni (Webinar) ni kueleza jinsi gani watafanikiwa kwenye biashara yako mbeleni. Mara nyingi tunaangazia sana kwenye kutengeneza maudhui makubwa ya semina ya mtandaoni (Webinar). Na kuyawalisha katika mtindo mzuri, jambo ambalo sio baya lakini hautumii muda mrefu kuonyesha hatua inayofuata.

Nini maana ya Semina ya Mtandaoni (Webinar)?

Semina ya Mtandaoni, ni mtindo wa semina au mkutano wa kibiashara, mauzo, matangazo unaofanyika mtandaoni.

Neno “Webinar” linatokana na maneno matatu yaani (Portmanteau of Web and Seminar) ikiwa na maana ya muhadhara, uwasisilishaji au semina inayosafirishwa au kupitishwa kwenye wavuti.

Kulingana na utafiti wa taasisi ya InsideSales.com, zaidi ya 73% ya meneja mauzo na masoko wanaona kuwa semina ya mtandaoni ni bora zaidi  katika kutengeneza idadi kubwa ya wafuasi. Kutokana na takwimu hizi haupaswi kuziacha tu zipite hivi.

Jinsi ya kumbadilisha mfuasi wa Semina ya Mtandaoni kuwa mteja

  1. Waulize maswali (Polling) wafuasi wako wa webinar kuona nani yuko tayari kununua

Fanya uchaguzi wa wafuasi wako kuona nani yuko tayari kununua. Kwenye Webinar/Semina ya mtandaoni mara nyingi hutumia njia kwa kuwauliza maswali wafuasi wake kama njia ya kuwaweka karibu na kampuni.

Kufanya uchaguzi au kutumia njia ya kuuliza maswali(Polling) kwenye webinar itakusaidia kujua kama wapo kwa ajili ya kujifunza kuhusu kampuni yako au kwa ajili ya kuongea tu na mwakilishi wa kampuni.

Kumbuka kuwafanyia mahojiano wafuasi wako wakati wa semina ya mtandaoni kutakupa muitikio mzuri kuliko kufanya baadae.

  1. Tuma utafiti wa Semina ya mtandaoni.

Kuwatumia wafuasi wako utafiti wa webina yako mara baaada ya kufanyika kwake ni njia nzuri ya kuwaonyesha kuwa maudhui yake yalipitiwa na wao na inaweza kukudaidia kupata wafuasi wengine.

Kama haukupata muda wa kuwauliza maswali hapo mwanzo, waulize sasa nani yuko tayri kuendelea na hatua inayofuata.

  1. Waingize timu yako ya mauzo kwenye Webinar yako.

Kuwaingiza watu wa mauzo kwenye webinar itawasaidia katika kupanga kalenda yao ya mauzo kwakuwa watakuwa wanajua ni mada gani inayowasilishwa kwenye webinar

  1. Fuatilia webinar yako ndani ya masaa 24

Jitahidi kutuma barua pepe za kwanza za mrejesho kwa wafuasi wako wa webinar kila baada ya masaa 24. Wafuasi wako watategemea kupokea sauti na video za maudhui uliyowasilisha kwenye webinar yako.

  1. Wajali wafuasi wako wote

Hata kama wafuasi wako wa webinar hawawezi kuwa wateja wako wa kununua bidhaa yako kwa sasa. Haupaswi kupoteza muda wa kuwafunga hata kama hawawezi kununua kwa sasa.

Mtumizi ya semina ya mtandaoni yanaleta wateja wako kwa ukaribu kujua kitu unachofanya ikiwa ni pamoja na bidhaa unayouza au huduma. Kwa msaada zaidi ili kuweza kukusaidia kuendesha biashara yako kwa njia ya kidigitali BONYEZA HAPA.