Kukuza Biashara

Kama mfanyabiashara siku zote unatizama katika upande bora zaidi, upande wa maendeleo. Hii ina maana siku zote unapenda kuiona Biashara  yako ikikua na kupanuka zaidi. Pia unaweza kuwahudumia wateja wengi zaidi na faida inazidi kuongezeka.

Biashara huanza kutanuka kuanzia chini kabisa. Nikimaanisha kwamba mteja aliye karibu na Biashara yako ndiye anayeweza kusema mema kuhusu Biashara yako, akaaminika zaidi kuliko tangazo lako lililogharimu zaidi ya milioni mbili kuruka hewani.

Kama wewe ni mfanyabiashara au Mjasiriamaliunayehangaika kukuza Biashara yako basi ukifanya njia hizi huenda mambo yakabadilika kwa kiasi kikubwa sana;

 

Biashara

  1. Ongeza Idadi Ya Wateja

Nafikiria unafahamu kuwa wateja ndio wanaokuingizia pesa katika Biashara yako. Na kila ukiwa na wateja wengi ndivyo kipato kinavyozidi. Na kila wanavopungua ndivyo kipato kinapungua na hatimae kuuwa Biashara yako.

Unahitaji kujitanua kwa kukuza network, kujuana na watu, kuungana na Biashara nyingine katika kutoa huduma zako. Jaribu kuwafanya watu wengi zaidi wakufahamu. Ziko njia nyingi sana za kufanya hivi lakini moja ni kuwa na mahusiano mazuri na wafanyabisahara wenzako.

Je Wateja Wako Utawapata Wapi?

Njia kuu ya kupata wateja ni kujitangaza. Wateja hawapatikani isipokuwa wewe au hata watu wengine kutangaza kwa watu kuwa una biashara fulani yenye kutoa bidhaa au huduma fulani.

Na matangazo unaweza kufanya kwa njia mbili.

  • BURE

Kuwa na ofisi sehemu iliyo mbele za nyuso za watu, kuongea na watu ana kwa ana, kutumia mitandao ya kijamii, kutumia marafiki au hata wateja kutangaza Biashara yako.

  • Kulipia matangazo

Hii itakusaidia kuwafikia maelfu ya watu kwa mpigo, kitu ambacho kitakusaidia kuongeza idadi ya wateja wapya mara moja.

SOMA ZAIDI: ONGEZA KIPATO

  1. Ongeza Idadi Ya Mauzo kutokana na Kila Mteja anayekufikia

Kama kila mteja anakuingizia wastani wa shilingi elfu kumi kwa kila manunuzi, inabidi ujitahidi kumshawishi mteja huyo kununua bidhaa za ziada zitakazokufanya uongeza mapato kwa kila manunuzi. Swala la kujiuliza ni bidhaa gani ya ziada unayoweza kuwauzia wateja wako juu ya kile kitu wanachonunua kila siku?

Kama wewe upo katika Biashara ya kuwatengenezea wateja wako tovuti. Basi watahitaji kusajiliwa domain name na kurushiwa tovuti yao hewani,  au watahitaji kutengenezewa hata logo kwa ajili ya Biashara zao.

Na uzuri ni kuwa haikugharimu pesa yoyote kwa kutumia mfumo huu kuongeza mauzo zaidi. Na hii unaweza kufanya katika biashara yoyote hata kama una kiduka kidogo cha kuuza vitu vya kuhitajika majumbani.

Biashara

 

  1. Ongeza Idadi Ya Mauzo Endelevu

Jambo la tatu la muhimu kufanya ni kuhakikisha wateja wako wanarudi kwako mara kwa mara kununua bidhaa au huduma unayotoa.

Unaweza kufanya hivi kwa Kuuza bidhaa au huduma inayopendwa zaidi na wateja wako au Kuwasiliana na wateja wako mara kwa mara kuwajulisha kuhusu OFA au bidhaa au huduma mpya unayotoa.

SOMA ZAIDI: ONGEZA MAPATO

 

  1. Tazama ni wapi unakosea na kufanya marekebisho.

Mara nyingi changamoto katika Biashara yeyote ile lazima zijitokeze.Hakuna binadamu ambaye amekamilika kukosea ni sehemu ya mafanikio ya kibiashara hivyo usigope pindi changamoto zinapojitokeza,na pindi tunapokosea ndipo tunapojifunza zaidi.Inawezekana Biashara yako haileti faida kutoka na wafanyakazi wako na vitu vingine jaribu kufanya uchunguzi wa kina na kuvirekebisha. Ili kukuza Biashara ni lazima ufanye tathimini ni mipango ipi inakuletea faida katika biashara? kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuuzingatia. Kwani sio kila mipango unayopanga huleta faida.

  1. Tambua Soko lako liko wapi

Katika Biashara hasa ndogondogo ni muhimu kufahamu soko lako liko wapi na kama bidhaa yako inaweza kujiuza. Utakapogundua ni wapi soko lako lilipo anzia hapo, ongeza juhudi, ubunifu na ustadi katika huduma unazozitoa huduma.

Je wewe unakuza na kutanua Biashara yako kwa kutumia njia gani?

Tujulishe kwa ku” comment” hapo chini bila ya kusahau ku bofya” share” ili na wengine wengi wafaidike.