Amini usiamini, hakuna kitu kinakatisha tamaa au kuchosha kama kuwasiliana na mteja mkorofi. Jambo la mwisho ambalo ungependa  kulifanya ni kuendelea kuongea nae tu. Najua ungependa kumuambia ni maneno gani yanafaa kutumika ambayo hayaleti msuguano baina yenu.

Kwa bahati mbaya hauwezi kufanya hivyo. Njia hiyo itakuletea shida wewe pamoja na kampuni yako katika maisha yajayo. Unapaswa kuudhibiti ulimi wako pamoja na kushusha hasira unapokuwa unamuhudumia mteja mkorofi.

SOMA ZAIDI:

Mteja mkorofi ni yupi?

Mteja mkorofi ni yule mteja ambaye mara nyingi anatumia lugha ya ukali, yenye kuudhi hasa anapokuwa anahisi ameshindwa kupata huduma au bidhaa kwa namna iliyostahili.

Namna ya kushughulika na mteja mkorofi

  1. Jifunze mazoezi ya kuwa mpole au kutuliza jazba

Kuna mbinu nyingi zinazoweza kukusaidia katika kutuliza jazba unapokuwa unamuhudumia mteja ambaye ni mkorofi.

Kwanza, jifunze kushusha pumzi (Deep breath). Jitahidi kufanya hivyo zaidi ya mara 10, ukivuta pumzi kupitia pua yako na kutoa pumzi kupitia mdomo wako. Hii inaweza kurekebisha mapigo yako ya moyo na kupunguza kabisa.

Pili, unaweza kutumia njia ya kufunga macho yako na kisha anza kuvuta taswira ya jambo Fulani ambalo linakufanya ujisikie mtulivu. Labada inaweza ikakuleta picha ya ukiwa kwenye fukwe Fulani au ya mtu uanayempenda sana. Picha hii itakufanya ujione uko kwenye kipindi Fulani cha furaha na itakupa wakati mzuri.

  1. Usijichukulie wewe mwenyewe (Don’t take it personally).

Kamwe haupaswi kujiweka wewe kama wewe kwenye maoni ambayo sio ya heshima, yenye kuudhi na yenye kukosoa. Muda mwingi, maoni ambayo mteja mkofi anayatoa hayamaanishi kuwa analenga kukushambulia wewe. Rahisi tu, wao huwa na hasira na wewe ndio mtu pekee waliyepata bahati ya kuongea nae.

Jiweke mbali na vile wanavyovisema, na jaribu kutambua kuwa wanakuwa wakali kuhusu bidhaa au huduma inayotolewa. Wanakuwa wkali na kampuni nzima na hata kama ikitokea kuwa wamekasirishwa na jambo ambalo wewe umeslisema, tambua kuwa kila mtu anafanya makosa. Unachopaswa kufanya ni kuchukua maoni yao na kujitenganisha na wewe binafsi na kazi yako.

  1. Kuwa na huruma (Be Empathetic)

Njia mojawapo ya kuwa mpole ni wewe kuvaa viatu vya mteja. Kuchukua nafasi ya mteja

Kwanza, hii inaweza kukuondoa wewe kwenye hali ya ubinafsi kwa kuangalia mitazamo ya watu wengine.

Pili, Vaa viatu vya mteja. Hii inaweza kukusaidia kuelewa wapi wametoka. Inaweza kukusaidia kuwa mpole kwakuwa utatakiwa kutambua kuwa hawewzi kuwa na hasira pasipo sababu maalumu. Wamepatwa na hasira kwakuwa walikuwa na imani na kampuni yenu lakini mmewaangusha.

Kuwa na huruma inaweza kukusaidia kuwalinganissha wateja na vitu gani wanahitaji kusaidiwa.

  1. Je, Sauti yako inalingana na hali yako ya utulivu

Sauti yako inaweza kutoa mbali hisia zako za kweli. Ni rahis sana kuongea kabla haujafikiria unapokuwa umekasirishwa na jambo ambapo itakuletea hofu na maneno yasiyo ya kawaida.

Jitahidi kuongea taratibu bila hata ya kupandisha sauti yako, hii inaweza kukusaidia kupa utulivu kati yako na mteja wako.  Jifunze mara kwa mara kujibu malalamiko au maoni kwa mteja kwa aina hiyo ya sauti.

  1. Jifunze kuomba Msamaha wa dhati na kweli

Ni kweli, unapaswa kuomba msamaha wakati wote uwe unajisikia kuomba msahama ama la. Maana kubwa ya kuomba msamaha ni kuonyesha kwa namna gani ulivyojisikia vibaya kwa mteja wako kushindwa kupata bidhaa au huduma ilivyotakiwa.

Lakini ukiwa kama muungwana, haupaswi kuomba msamaha kwa mteja kama jambo linalolalamikiwa halikufanyika kwenye kampuni yako. Kuomba msamaha kutakupelekea wewe kukiri makosa ambayo kampuni yako hayajayafanya. Hivyo basi unapaswa kuwa makini na lugha yako.

Jairbu kutumia kauli kama hizi Samahani kwakuwa umepata bidhaa sivyo ndivyo” lakini usitumie kauli hizi, “Samahani kwa kile kilichotea” au “Samahani tulikosea kufanya hilo”

  1. Zingatia kutafuta suluhisho la mzizi wa tatizo

Mteja anavyokutolea maneno ya kuudhi, ni rahisi kupoteza mwelekeo wa kujua tatizo ni lipi? Unapaswa kuwa mpole. Zingatia sana kwenye tatizo badala ya kulenga kile anachokisema. Mara unapotambua tatizo ni nini? Inakuwa rahisi kwako kutatua tatizo.

Somo unalopaswa kujifunza unaposhughulika na mteja mkorofi ni kuwa mara nyingi huwa wanapenda kutoa hasira zao kwako. Inakuwa ni ngumu kwako kulipokea hilo kama mtu wa mwisho lakini hauwezijua maisha halisi ya mteja wako. Wakati mwingine huwa wanapambana na hali za maisha yao kama vile matatizo ya kifamilia au kupoteza kazi. Mwisho wa siku, kazi yako ni kufanya maisha yao yawe rahisi zaidi kwa kutatua matatizo yao yanayowakumba wanapotaka kununua bidhaa au huduma yako.

Unaweza kujifunza mengi na hata kutafuta njia mbadala za kidigitali za jinsi gani unaweza kushughulika na wateja wako katika hali ya utulivu. Unaweza kutufuata kupitia mitandao yetu ya kijamii kupitia ukurasa huu au BONYEZA HAPA kwa mawasiliano zaidi.