Ili kufanikiwa kwenye biashara kwa sasa ni wazi unahitaji kuwa na mawazo chanya, mipango mizuri pamoja na mpangilio mzuri wenye ustadi. Watu wengi uanzisha biashara au kufungua tu ofisi wakiamini kuwa wanaenda kutengeneza tu pesa na baadae wanakuja kugundua kuwa kutengeneza fedha kwenye biashara sio rahisi kama walivyofikiria.

Lakini wewe unaweza kuepuka ili kwa kutengeneza mipango thabiti ya biashara yako. Wapo vijana wengi ambao wamejaribu kutengeneza mawazo yao ya biashara na kuyaweka kwenye uhalisia na kisha kuyafanyia kazi.

Kwa mfano, Idrisa Ayoub maarufu kama “Muuza Uji”. Kijana aliyetambulika kwa biashara ya uji, biashara ambayo tumekuwa tukiiona kwa akina mama wengi ambao wanatembea na chupa zao za Uji.

Idrisa amaejaribu kutengeneza mchanganyiko mzuri wa bidhaa mbalimbali akiita “Wakanda Mix” na kuleta utofauti na biashara nyingine ya uji tuliyoizoea mtaani. Lakini pia tusisahau matumizi ya mtandao pia yanaifanya biashara hii kuonekana kwa urahisi na kutengeneza wateja wengi.

Ni wazi kuwa na wazo kama hii unahitaji kuwa na mipango kazi na mikakati ya jinsi biashara yako inavyoweza kwenda kwa ufanisi.

Carpets zuliatz ni miongoni pia ya wafanyabiashara ambao wanajitahidi kupanga mawazo yao na kuyaweka katika mtindo wa kipekee wenye kumfanya mteja ajisikie anaweza kupata huduma au bidhaa kwa urahisi na haraka. Yeye ujihusisha na biashara ya kuuza mazulia mbalimbali ya ndani, lakini kwa kiasi kikubwa utumia mitandao kuifanya biashara yake kuonekana kwa urahisi.

Hivyo ni wazi ili ufanikiwe Katika biashara yako unahitaji kuwa na mpangilio mzuri wa mawazo yako ya kibiashara.

Njia za kufanikiwa katika mawazo yako ya biashara.

1.     Jipange

Ili kufanikiwa katika biashara unahitaji kujipanga. Kujipanga kutakusaidia kukamilisha mipango yako na kukaa kwenye malengo ya biashara yako. Na njia nzuri ya kufanya hilo ni kuwa na orodha ya mpangilio wa shughuli zako. Hii itakuwezesha kufanya vitu vyako kwa mtiririko na utaratibu ulio na tija. 

2.     Weka kumbukumbu zako kwa kina

Wafanyabiashara wote waliofanikiwa huwa wanarekodi  taarifa zao kwa ustadi. Hii itakufanya kujua wapi biashara yako imesimama kifedha na ni changamoto gani zinakukabili. Kuhamu hilo itakusaidia kuwa na mikakati mizuri ya biashara yako. 

3.     Changanua Mshindani wako

Ushinadani katika biashara unaleta matokeo chanya. Ili uweze kufanikiwa katika biashara haupaswi kuogopa kujifunza kutoka kwa wapinzani wako. Wanaweza kukupa kitu ambacho kinaweza kukusaidia kwenye biashara yako. 

4.     Tambua Faida na Hasara (Risk & Reward).

Njia bora ya kupima mafanikio ya biashara ni kuhesabu hasara. Swali unalopaswa kujiuliza ni “Nini maana ya kushuka kibiashara” ukiweza kujibu swali hili utaweza sasa kujua mazingira ya hali mbaya ya kibiashara. 

5.     Kuwa mbunifu.

Wakati wote unapaswa kutafuta njia ya kuboresha biashara yako na kuweza kusimama kwenye soko la ushindani. Tambua kuwa hauwezi kujua kila kitu na kuwa wazi kujifunza mawazo mapya ya kibiashara na njia mpya za kibiashara. 

6.     Kuwa mvumilivu.

Kuna msemo huwa unasemwa kuwa, “Roma haikujengwa siku moja”. Sio kwa sababu tu umefungua biashara basi utaweza kutengeneza pesa papo kwa papo. Inachukua muda kwa watu kufahamu nini unafanya? Kuwa mvumilivu katika kutimiza malengo yako. 

7.     Jiandae kujitoa  mhanga

Mwongozo wa kufungua biashara ni kufanya kazi kwa bidii, mara tu baada ya kufungua milango yako basi na kazi imeanza. Unapaswa kuweka juhudi sana kwenye biashara yako. 

8.     Toa huduma iliyobora kwa wateja

Wapo wafanyabiashara wengi waliofanikiwa ambao wanasahau kuendelea kutoa huduma bora kwa mteja ni jambo la umuhimu. Kama utakuwa unatoa huduma nzuri kwa mteja kuna iuwezekano wa asilimia mkubwa mteja kuwa wa kudumu au kukutafutia wateja wengine 

9.     Kuwa na mwendelezo sawa (Be constitent)

Kuwa naz mwendelezo ulio sawa kwenye biashara yako ndio dhana kubwa ya kuendelea kutengenza fedha kwenye biashara yako. Unapaswa kuendelea kufanya kinachohitajika katika shughuli zako zote za biashara za kila siku. Hii itakutengenezea tabia chanya ya muda mrefu kwenye biashara yako ambayo itakusaidia kuendelea kutengeneza fedha.

Kama unahitaji biashara yako iweze kufanikiwa basi unahitaji kufuata hatua hizo tisa. Hatua ambazo zitakuepeleka kwenye ufunguo wa mafanikio ya biashara yako.

Kwa msaada zaidi kuhusu jinsi ya kuifanya biashara yako iweze kukua zaidi ya hapo kwa zaidi ya 50% kupitia digital Platform tutembelee kwenye website yetu tukusaidie au BONYEZA HAPA. Ikiwa ni pamoja na kukupa ushauri na mawazo chanya yatakayoijenga biashara yako na kuifikisha mbali.