Zipo njia mbali mbali za kukusanya maoni ya wateja. Mara nyingi njia ya utafiti (Survey) ndio njia inayokuja kwa haraka unapokuwa unafikiria ipi ni njia nzuri. Lakini hiyo sio njia ya mbadala ya kutambua kile ambacho wateja wako wanasema kuhusu bidhaa yako.

Mitandao ya kijamii ndio njia yenye tija pale unapokuwa unahitaji maoni kutoka kwa mteja kuhusu bidhaa au huduma. Kupitia idadi kubwa ya watumiaje wake  ulimwenguni kote ambao tayari wamejiunga na mtandao huo wa kijamii. Unapaswa kuwa na wasifu wenye maelezo ya kutosha na kutoa msaada wa kutosha kupitia brand ya biashara yako kwa wateja. Wateja ambao ni thamani kwako na wanahitaji huduma kwa urahisi na kwa haraka.

Zaidi ya hapo, ni muhimu kujua nini wateja wako wanazungumza kuhusu biashara yako kwenye mitandao ya kijamii. Kwa sababu kama watu zaidi ya million wanaotumia mitandao ya kijamii ambao ni wateja wako wapya muhimu wataona taarifa mbaya kuhusu huduma zako au bidhaa zako basi basi ni rahisi tarrifa hizo kusambaa kwa haraka na kuharibu kabisa biashara.

Nini Maoni ya mteja (Customer Feedback)?

Maoni ya mteja ni taarifa inayotolewa na mteja kuhusu kama wameridhishwa na bidhaa au huduma walipokea au hawajaridhishwa pamoja na uzoefu wa jumla waliokuwanao kuhusiana na kampuni au biashara husika. Taarifa hizi ni muhimu sana katika kutengeneza uzoefu wa mteja kwenye biashara yako pamoja na kuchukua hatua kulingana na mahitaji yao.

SOMA ZAIDI:

Nawezaje kutumia mitandao ya kijamii kupata maoni ya wateja wangu?

  1. Kusikiliza na kufuatilia majadiliano ya wateja.

Jitahidi kufuatilia mazungumzo ya kuhusu biashara yako pamoja nay ale kuhusu mpinzani wako kibiashara. Kwa kushiriki kwenye mazungumzo yanayohusu biashara yako kwenye media unaweza kupata msaada kutoka kwa wateja hapo hapo pamoja na maoni ya juu watu wanavyozungumza kuhusu huduma au biashara yako pasipo kuzingatia kama waliwasiliana na wewe moja kwa moja.

Lakini pia kwa kufuatilia mazungumzo ya kiushindani unaweza pia kufahamu wateja ambao hawafurahii kuhusiana na bidhaa nyingine ya mshindani wako. Jiulize kwanin hawaridhiki halafu jifunze ili uweze kuwatafutia ufumbuzi .

  1. Kukusanya maoni ya bidhaa yako.

Unapotaka kutoa bidhaa mpya au unafanya mabadiliko ya muonekano wa bidhaa yako iliyopo kawaida unategemea kupungua kwa idadi ya wateja wako wa sasa.

Unaweza kutumia mtandao wako kabla ya kufanya maamuzu au mabadiliko yeyote yale kuomba maoni kwa wateja wako waaminifu kwenye biashara yako. Kitu kikubwa katika mitandao ya kijamii, haiuishi tu wateja wako wa kila siku bali pia wateja ambao ndio walengwa wa kesho.

Kupata maoni yenye wigo mpana kuhusu muonekano mpya wa bidhaa zako. Iwe katika urahisi wa kutumia au imeendelezwa vizuri itakusaidia katika maendeleo ya biashara yako.

  1. Kupitia Makundi Mbalimbali ya mitandaoni.

Uwepo wa makundi mbalimbali ya mitandaoni yanaweza kugawa wateja kwenye makundi mablimbali. Kwa sababu Makundi yanahitaji watu ambao wanaweza kutoa maoni wanatoka kwenye daraja au sifa za aina moja hivyo ni njia nzuri katika kupata maoni yenye tija.

  1. Endesha utafiti na kura za maoni.

Omba watu kwenye mitandao ya kijamii wakupatie maoni yao kwenye jambo lako la msingi kupitia njia ya utafiti au kura za maoni. Inaweza lisiwe jambo la zito sana likawa jambo jepesi ambalo litakupa uwezo wa kuhulisa maswali mepesi kwa ajili ya kupata maoni kuhusu mapendeleo ya mteja.

Hii ni njia ya pekee sana na inahusisha kutafuta maoni ya mteja. Maoni ambayo ni tofauti na ya barua pepe na ujumbe mfupi wa maandishi.

  1. Kuunganisha maudhui yako ya blogu na mitandao ya kijamii.

 Kuwa na maudhui yako ya kwenye blogu yako kwenye mitandao ya kijamii. Maoni ya wateja wako na watu wengine kwenye mitandao yako yatakusaidia kujua ni maudhui gani ni bora kwa wateja wako. Na maudhui yapi mabaya kwenye biashara yako.

Licha ya kuwa maoni ya kwenye mtandao yanaweza kuwa sio rahisi kwako. Tofauti na ingekuwa ya kwenye barua pepe au ujumbe mfupi au ya kupitia simu. Wakati mwingine uwazi unaweza kuleta thamani na kukupa maoni yenye tija kutokana na majibu ya msuguano ya wateja.

Hivyo basi ni wazi kama unaweza kuitumia vizuri mitandao ya kijamii unaweza ukapata faida kubwa katika kukuza na kuendeleza biashara yako katika hali ya kifanisi.

Hili kuweza kupata taarifa mbalimbali  pamoja na huduma zetu mbalimbali kwenye masuala ya biashara, App za simu, matumizi ya mitandao ya kijamii kwenye biashara na mengine mengi. Bonyeza HAPA kwa mawasiliano zaidi