Ni wazi sasa Teknolojia imekua kwa kiasi kikubwa. Ukuaji wa Teknolojia si tu umerahisisha mifumo ya kibiashara bali hata kuleta ufanisi hata katika sekta nyingine kama vile Elimu katika kujifunza au kujisomea Afya na kadhalika.

Moja ya mambo makubwa kwa mwanadamu ni kwamba hutaacha kujifunza. Na jambo kubwa juu ya kuwa hai leo ni kwamba kiasi kikubwa cha kujifunza kinapatikana bure, kwenye mtandao. Aidha unataka kujifunza juu ya historia yako, au kuwajenga watoto wako katika kujifunza, au kuongeza ujuzi au wasifu mpya kwenye wasifu wako wa zamani (CV) .

Kuna programu mbalimbali ambazo hutolewa Duniani kwa ajili ya wewe kujifunza. Mara nyingi programu hizi hutolewa na taasisi za juu za Dunia. Unaweza kupata kozi na ratiba ya darasa zilizowekwa na baadhi ambayo ni ya kujitegemea kabisa. Sasa programu zinampa mtu fursa ya kuweza hadi kutunukiwa shahada ya mtandaoni baada ya kumaliza kozi.

SOMA ZAIDI:

Hizi ndizo kurasa bora za kujisomea Mtandaoni

  1. Khan Academy

Khan Academy ni taasisi isiyo ya kibiashara ambalo lina msemo usemao “Unaweza kujifunza kitu chochote, bure, kwa kila mtu. Milele. “ Khan hutoa kozi hasa hasa katika ngazi ya msingi na ya sekondari, lakini pia kuna majaribio kadhaa ambayo wanayatoa kutokana na kozi mbalimbali kama vile, LSAT, au MCAT kwa elimu ya ngazi ya wahitimu. Na linapokuja suala la kompyuta, unaweza kupata msingi imara katika ujuzi kama HTML, CSS, SQL, na JS bila kulipa fedha yoyote.

  1. Open Culture Online Courses

Open Culture imewekeza zaidi ya kozi za bure 1,300 mabazo utazipata mtandaoni. Nyingi kati ya hizo zinatoka kwenye vyuo vikuu vinavyoongoza Duniani kama vile Stanford, Yale, MIT, Harvard, Berkeley, na Oxford. Upitia Open Culture utajifunza kuhusu uchumi, historia, fasihi, lugha, falsafa, sayansi ya kisiasa, biolojia, kemia, uhandisi, sayansi ya kompyuta – orodha inaendelea na kuendelea.

Kozi zote ni bure, lakini kwa sababu zinatoka kwenye vyuo vikuu tofauti, zina vipengele tofauti na mahitaji ili kukamilsha. Baadhi zikiwa na mkusanyiko wa mihadhara ya video kwa wewe kujifunza kwa kasi yako mwenyewe.

  1. Academic Earth

Hii ni tovuti nyingine ambayo imekusanya mkusanyiko wa kozi za bure kutoka vyuo vyuo vikuu bora . Chuo kama MIT inaongoza kwa kuwa na kozi zaidi ya 232, lakini shule kama Berkeley, Stanford, na Yale pia hutoa chache sana.

Academic Earth ilianzishwa mwaka 2009 kwa msingi kwamba kila mtu anastahili kupata elimu iliyobora. Kupitia tovuti yao, Inakuwezesha kuchagua masomo au shule. Zaidi ya kozi za bure, pia kuna taarifa za kutosha kuhusu jinsi ya kupata shahada ya mtandaoni kwa maeneo yote yanayojumuisha jumla ya kozi 10 pamoja na michepuo mbalimbali.

  1. Open2study

Hii ni tovuti iliyoko nchini Australia na inatoa karibu kozi 50 za bure kupitia vyuo vikuu vya Australia. Hili ni chaguo zuri sana hasa ikiwa hauna muda mwingi wa kukamilisha kozi yako ukiwa chuo ama la kwa kuwa itakuhitaji zaidi ya mwezi mmoja tu kumaliza kozi. Kutakuwa na Assignment na quiz kadhaa huku ukihitajika kukamilisha wastani angalau 60% ili kupokea cheti. Open2Study hutoa kozi za Usimamizi wa Mradi, Kuandika, na Mipango ya Fedha n.k.

  1. Codecademy

Lugha ya Kompyuta (Coding) ni ujuzi muhimu sasa na utakuwa muhimu zaidi kadri miaka inavyoendelea. Codecademy inafundisha coding bure, na kwa kipindi chake chote imefanikiwa kutoa wahitimu ambao wamekwenda kufanya kazi katika makampuni mbalimbali makubwa Duniani kama Facebook, Google, Bloomberg, na IBM. Jambo kufurahisha, kozi zake nyingi zinaweza kukamilika kwa siku kadhaa tu.

Suala la teknolojia mpya linaleta mafanikio makubwa katika nyanja nyingi sana. Deep Media wanakupa nafasi ya kuonana na Its wao kwa ajili ya kupata Programu mbalimbali iwe kwenye kampuni au biashara kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa biashara yako.

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA.