Maisha ya sasa mnunuzi anakuwa na nguvu kubwa inapofika wakati wa kufanya maamuzi ya kununua bidhaa au hata huduma. Unapaswa pia kufahamu kuwa mara nyingi huwa wanafanya utafiti wao kupitia mtandaoni. Lakini unapaswa kujiuliza, je, umejaribu kuweka mfumo wa mipango yako ya masoko unaoendana na mfumo wa mnunuzi wa bidhaa wa nyakati hizi?

Takwimu za aina 3 za tabia za mteja wa nyakati hizi.

  • 80% ya watuamiaji wa instagram wanazifuata akaunti za instagram za kibiashara, hii ni kutokana na taarifa za mtandao wa instagram 2017.
  • 75% ya watumiaji wa sikanu (smartphone) kitu cha kwanza kukifanya wakiwa mtandaoni ni kutafuta anuani ya akaunti husika kwa ajili ya kutoa mahitaji yao. Hii ni kutokana takwimu za mtandao wa Google 2018.
  • Barua Pepe zote ambazo hazijitokezi kwa uzuri na urahisi kupitia simu za mkononi huwa zinafutwa ndani ya sekunde 3 tu. Hii ni kutokana na taarifa za mtandao wa HubSpot.

Swali la kujiuliza ni kuwa, ni vitu gani mtu anayeshughulika na masoko anapaswa kuvifanya ili kuhakikisha kuwa mteja anakupata kwa urahisi na mara kwa mara? Ni kiasi gani unauelewa kwa ufasaha kuhusu wapi mteja wako anafanya utafiti wake na vitu gani vinavyomshawishi yeye kufanya maamuzi?

Hapa ndipo utafiti wa masoko unapoanza kuchukua nafasi yake. Haijalishi wewe ni mgeni au una uzoefu kwenye kufanya utafiti wa masoko, muongozo huu utakupa njia na ramani ya kukuongoza katika kujifunza kuhusu bidhaa, mteja mlengwa, na mambo mablimbali kwenye biashara yako.

SOMA ZAIDI:

Aina za Utafiti wa Masoko

Kuna aina mbili za utafiti wa Masoko ambazo kwenye biashara yeyote hutumika kama njia ya kukusanya taarifa kuhusu bidhaa yake. Nazo ni

  1. Utafiti wa Msingi/awali (Primary Research)
  2. Na Utafiti wa Pili/Sekondari (Secondary Research)
  1. Utafiti wa Msingi (Primary Research)

Huu ni aina ya utafiti ambao unazingatia kutafuta taarifa za msingi kuhusiana na bidhaa yako pamoja na wateja wake. Aina hii ya utafiti unaweza kutumia vikundi mbalimbali, utafiti wa mtandaoni, mahojiano ya simu,zaidi katika kupata taarifa kuhusiana na vikwazo ambavyo wateja wako wanakutana navyo ikiwa pamoja na uelewa kuhusu jina la biashara yako (Brand awaereness).

Utafiti huu unatumika zaidi has pale unapokuwa umegawa wateja wako kulingana na tabia zao, na unaweza kuangukia kwenye moja ya aina mbili za utafiti yaani.

  • Utafiti wa kimaelezo (Explanatory Research)

    Aina ya utafiti wa msingi wa kimaelezo ambao hauhusiani sana na kupima mwenendo wa mteja pamoja na matatizo ya mteja mara nyingi hutumia mfumo wa maswali ya wazi kwa mteja pamoja na utafiti kwa kikundi cha watu wachache.

  • Utafiti maalum (Specific Research)-

    Ni aina ya utafiti wa msingi ambao unafuata utafiti wa kimaelezo na unatumika kuangalia mambo muhimu katika biashara. Katika aina hii ya utafiti mtafiti anaweza kuchukua sehemu ndogo ya kikundi cha watu ambao aliwagawa kutokanana na tabia zao na kuwauliza maswali ambayo yatakwenda kutatua matatizo yao.

  1. Utafiti wa pili/sekondari (Secondary Research)

Huu ni aina ya utafiti wa masoko ambao unakusanya taarifa zote ulizozikusanya kwa ajili ya kutengeneza suluhisho. Hii inajumuisha taarifa za mwenendo, takwimu za masoko, pamoja na taarifa zote za mauzo kwenye biashara yako.

Aina hii ya utafiti ni bora zaidi katika kufanya uchambuzi wa washindani wako katika biashara. Kuna iana tatu za vyanzo vya Utafiti wa pili.

  • Vyanzo vya Umma (Public Sources)-Mfano takwimu za kiserikali pamoja na takwimu mbalimbali
  • Vya kibiashara (Commercial Sources)-Huusisha ripoti za masoko, na taarifa mbalimbali kuhusiana na biashara.
  • Vyanzo vya ndani (Internal Sources)-Huusisha taarifa zote ambazo taasisi husika inamiliki katika ofisi yake.mfano wastani wa mapato kwa kila mauzo n.k.

Jinsi ya kufanya utafiti wa Masoko.

Ili uweze kufanya utafiti wa masoko katika njia za kifanisi unapaswa kupitia hatua hizi.

  1. Mtambue mteja wako (Buyer Persona)

Kabla haujaanza kuwaangalia wateja wako kwenye biashara au kampuni yako kwa kuangalia vitu gani vinawashawishi kufanya maamuzi, unapaswa kutambua wateja wako ni wapi? Na wawakilishi wa wateja wako ni wapi?

 Mteja (Buyer Persona)-hili ni kundi la kufikirika la linalowakilisha wateja wako. Wanakupa uwezo wa kupata taswira ya wateja wako.kukusaidia katika mawasiliano yako pamoja na mpangao yako. Hawa huwa wanapatikana kutokana na sifa zaifuatazo.

  • Umri
  • Jinsia
  • Mahali
  • Kazi
  • Ukubwa wa familia
  • Kipato
  • Changamoto kubwa
  1. Tambua sehemu ya mtu atakayehusika miongoni mwao katika utafiti wako

Hatua ya kwanza umefanikiwa kujua nani mteja wako, nani anawakilisha kundi la wateja wako. Sasa unapaswa kuchagua baadhi ya watu kama sampuli watakaokuwa wanawakilisha wateja wako hili kujua tabia zao, changamoto wanazozipata na tabia za ununuzi. Unaweza kutumia njia ya makundi, mahojiano ya simu na hata utafiti wa mtandaoni.

Chagua mteja yupi anafaa kumfanyia utafiti

Unapokuwa unafanya uchaguzi wa sampuli unapaswa kuwa makini. Unaweza kutumia njia kadhaa kupata sampuli halisi. Tumia njia kama

  • Chagua wawakilishi 10 kwa kila kikundi cha wateja wakilishi
  • Chagua watu ambao walikuwa na mawasiliano na wewe katika biashara yako kupitia njia mbalimbali.
  • Zingatia katika kuchanga washiriki wako (Hapa unaweza kutumia wale waliohusika katika kununua bidhaa yako na wale waliohusika kutumia bidhaa ya mshindani wako.
  1. Wahusishe washiriki wako kwenye utafiti wako

Zipo hatua za kuwashirikisha washiriki wako kwenye utafiti unaotarajia kuifanya. Nazo ni

  • Chukua orodha ya wateja waliofanya manunuzi kwa siku za karibuni
  • Chukua orodha ya wateja waliokuwa wanajihusisha na biashara yako lakini hawajafanya manunuzi hivi karibuni.
  • Ita washiriki kupitia mitandao ya kijamii
  • Angalia msukumo-Jinsi gani unaweza kuwahamasisha watu watumie dakika 30-45 kwenye biashara yako na utafiti unaoufanya.
  1. Andaa maswali yako ya Utafiti

Jinsi nzuri ya kuepuka kujiweka kwenye mazungumzo ni kujiandaa. Unapaswa kutengeneza muongoza wa utafiti wako katika kila njia.

Hii haimaniishi kuwa lazima kuwepo na muswada la asha, mazungumzo yanfaa yawe ya kiasili zaidi.

Mwongozo wa ukusanyaji wa taarifa zako unapaswa kuwa hivi.

  • Taarifa za asili ya biashara (background information) dakika 5
  • Ufahamu (Awareness) dakika 5
  • Vya kuzingatia dakika (Consideration) 10
  • Maamuzi (Decisions) dakika 10
  • Kufunga (Closing)
  1. Orodhesha washindani wako wa msingi

Unapaswa kuwajuwa washindani wako, ukianzia na mshindani wa pili au wa sekondari na Yule mshindani nwa msingi.

Wakati mwingine unapaswa kujua mgawanyo wa ndani ya kampuni unaweza kutengeneza ushindani kwenye bidhaa kuu.

Ukizingatia taratibu hizo kwa kiasi kikubwa utakuwa umepata taarifa za msingi katika ufahamu juu ya utafiti wa masoko. Kwa kupata maelezo na njia mbadala hasa katika Nyanja ya kidigitali, wasiliana nasi kwa msaada zaidi kwa kubonyeza HAPA.