Kwanini biashara nyingi ndogondogo zinashindwa kuendelea?

Kushindwa katika biashara sio jambo la kufikiria unapokuwa unataka kuanzisha biashara. Takwimu iliyotolewa mwaka 2017 na Tasisi ya uongozi wa biashara ndogondogo (SBA) inaonyesha kuwa zaidi ya 30% ya biashara zinazoanzishwa huwa zinakufa katika mwaka wa kwanza tu wa kuanzishwa kwake huku 50% zinadumu kwa miaka 5 tu na 60% zinadumu kwa miaka 10.

Nini maana ya kufa kwa biashara?

Kufa kwa biashara ni hali inayojitokeza mara baada ya kampuni au biashara kusitisha shughuli zake za uendeshaji kufuatia kushindwa kutengeneza faida au kuleta mapato ya kutosha kwa ajili ya kufidia gharama za uendeshaji. Hata kampuni inayotengeneza faida inaweza kufa endapo tu itatengeneza faida ambayo inashindwa kufidia gharama za uendeshaji wake.

SOMA ZAIDI:

Ni sababu gani ambazo zinachangia biashara nyingi kufa?

Zipo sababu nyingi zinazosababisha biashara nyingi kushinndwa kuendelea. Zinaweza kuwa za kisiasa, kiuchumi kama vile kodi, lakini pia ukosefu wa amani, masuala kama vita ni moja ya sababu zinazowesha kusababisha biashara nyingi kushindwa kuendelea. Zifuatazo ni sababu za biashara nyingi ndogondogo kufa.

  1. Kuanza biashara ukiwa na sababu potofu.

Je, umeshawahi kujiuliza nini sababu ya msingi ya kuanzisha kwa biashara yako? Je, umeanzisha biashara yako kwa ajili ya tama ya kutengeneza pesa nyingi?

Jitahidi kupanga mikakati mizuri ya biashara yako hasa kuandaa mipango kabla ya kuanza kwa biashara.

  1. Uongozi mbovu katika biashara.

Ripoti nyingi za kufa kwa biashara zinaonyesha kuwa uongozi mbovu ndio chanzo kikubwa kwa biashara nyingi hususani ndogondogo kushindwa kuendelea.

Kama uongozi uliopo utashindwa kutambua nini matakwa ya biashara? Hali ya kibiashara ikoje?  Kwanini kampuni au biashara haifanyi vizuri na haitamaye kuomba usaidizi bado ni wazi biashara itashindwa kuendelea.

Viongozi wengi kwenye biashara ndogondogo wanaosa ujuzi katika maeneo ya kifedha, ununuzi, mauzo na hata uzalishaji.

Inapaswa kabla ya kuanzisha na hata baada ya kuanzishwa kwa biashara, mmliki wa biashara na wafanyakazi wapewe ujuzi katika Nyanja muhimu za uendeshaji wa biashara.

  1. Mtaji Mdogo (Insufficient Capital)

Kosa kubwa katika kuanzisha biashara ni kuwa na mtaji mdogo kwa ajili ya uendeshaji. Wengi wanaonza biashara hawajui mzunguko wa fedha ukoje au makadirio ya kiasi gani watatumia katika kuanzisha biashara. Mara nyingi wanakuwa na matarajio yasiyo na uhalisia ya kuingiza fedha nyingi kutokana na mauzo.

Ni vizuri kuanza kujiuliza ni kiasi gani cha fedha kitahitajika kwenye biashara unayotaka kuanzisha? Unapaswa kujua sio tu gharama za kuanzisha biashara yko bali hata gharama za kuendesha biashara yako katika siku zijazo. Ni uhalisia kuwa biashara nyingine zinachukua zaidi ya mwaka kuonyesha thamani.

  1. Kutokuwa na matumizi ya mtandao/digitali kuendesha biashara yako.

Ni jambo la umakini sana katika maisha ya kibiashara ya wakati huu. Kama umedhamiria kukuza biashara yako kwa ajili ya mapato zaidi basi hauwezi epuka matumizi ya Tovuti pamoja na mitandao ya kijamii.

Mfano nchini Marekani idadi ya watu wanaotumia mtandao au mdahalisi (Internet) inakadiriwa kuwa ni zaidi ya 85% ya watu wote.

Nchini Tanzania ni zaidi ya watu Milioni 23 kati ya idadi ya watu waote wanatumia mtandao kupata huduma mbalimbali.

Inashauriwa kuwa mfanyabiashara ili aweze kutoa huduma zake kwa mawanda mapana basi matumizi ya mtandao ni suala la kulizingatia. Mfanyabiashara anatakiwa awe na tovuti itakayomrahisishia kufanya biashara yake kwa haraka na kwa ufanisi ikiwa pamoja na kutengeneza wateja popote ulimwenguni.

Lakini pia mfanyabiashara anapaswa kumiliki akaunti za mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutangaza biashara yake kwa kiwango kikubwa zaidi.

  1. Kukosekana kwa mipango thabiti.

Kila biashara  inahitaji mipango thabiti. Ili uweze kuendelea na biashara yako katika hali ya utulivu unapaswa kuwa na mipango thabiti ya biashara yako inayobeba vitu kadhaa kama vile

  • Maelezo ya kina kuhusu biashara yako, maono na malengo
  • Uchambuzi wa Masoko
  • Nguvu inayohitajika hasa wafanyakazi
  • Matatizo yanayotegemewa pamoja na ufumbuzi
  • Masuala ya fedha
  • Kuangalia ushindani.
  • Kujitangaza pamoja na
  • Bajeti

ili kuweza kuifanya biashara yako ikue na kuweza kukuingizia mapato kwa zaidi ya 50%  hauna budi kuipeleka biashara yako katika nyanja ya kidigitali.Matumizi ya Tovuti pamoja na mitandao ya kijamii itakusaidia katika kuinua baishara yako. ili kuweza kupata uashauri na kujipatia Tovuti (Website) kwa gharama nafuu wasiliana na Deep Media kwa kubonyeza HAPA.