Unapofanya kazi katika biashara ndogo na huku ukiwa na bajeti ndogo, ni vigumu kutumia zaidi la dolla 340,000 kwa ajili ya tangazo la sekunde 30 kwenye Televisheni kwa ajili ya biashara yako. Au kutumia zaidi ya dolla 10,000 kwa ajili ya kufanya kampeni ya masoko kupitia barua pepe.

Inaweza kuwa jambo la kushagaza sana wakati bajeti yako inaelezea watu wangapi ambao biashara yako inaweza kuwafikia.

Jambo jema ni kuwa kuna njia nyingi za bure zinazoweza kuziba pengo la gharama unazolipa kwa ajili ya matangazo. Unaweza sasa kuingiza mbinu za matangazo ya bure kwenye mkakati wako, ili uweze kuondoa baadhi ya gharama zisizohitajika.

SOMA ZAIDI:

Njia za kupata matangazo bure kwenye biashara yako.

  1. Tumia “Google My Business” kuboresha utafutaji wa biashara yako.

Mojawapo ya njia zenye nguvu zaidi za kutangaza biashara yako ni kupitia “Google My Business” ambayo inaruhusu makampuni kusimamia uwepo wao kwenye “Google Search” pamoja na Ramani za Google (Google Maps).

Google My Business inaweza kuimarisha nafasi ya kuonekana kwako katika matokeo ya utafutaji. Kuonekana juu (High ranking) katika utafutaji unaonyesha kuwa wewe ni kampuni halali na inayofaa.

“Google My Business” ni nini?

Google My Business ni huduma ya msingi ya wavuti kwa wamiliki wa biashara ambayo inaendeshwa na Google. Inaruhusu wamiliki wa biashara kutoa habari ambazo zinaweza kuonekana kwenye “Google Search” kama vile saa za kazi, anwani, nambari ya simu, na picha.

Google inaweza kuchanganya habari zinazotolewa na mfanyabiashara na habari kutoka vyanzo vingine, ikiwa ni pamoja na tovuti ya biashara, msaada kwa mtumiaji wa Google, na tovuti za watu wengine.

  1. Tumia mtandao wa Yext kudhibiti taarifa zako

Kadri Sehemu nyingi zaidi biashara yako ilivyoorodheshwa mtandaoni, na uwezekano wako wa kuonekana juu kwenye Google Search ni mkubwa na hivyo ni rahisi wateja wako kukupata.

Ili kuhakikisha kuwa SEO (Search Engine Optimization)  yako inakwenda vizuri, maelezo ya orodha yako kwenye kila tovuti na ya mtandaoni yanahitajika kufanana. Kwa mfano, ikiwa tovuti yako inataja nambari ya simu mpya ya kampuni yako, lakini Yelp inataja namba yako ya zamani, hali hii inaweza kuathiri SEO yako.

Unashauriwa kutumia mtandao wa Yext ambao utakuwezesha kudhibiti taarifa zako kwa urahisi. Yext inatathmini mtandao ili kupata kila mahali ambapo biashara yako imeorodheshwa, hivyo unaweza kudhibiti orodha zako ili uhakikishe usahihi wake.

  1. Tumia Video za Youtube.

YouTube ina watumiaji zaidi ya bilioni moja, ambayo inakaribia theluthi moja ya watumiaji wa internet. Huku zaidi ya 59% ya watendaji ambayo ufanya maamuzi hutumia maudhui yaliyoko kwenye mtandao huu wa Youtube.

Jitahidi kutengeneza maudhui ya video za YouTube zenye ushiriki na zenye kutoa taarifa kama njia mojawapo ya kujenga ufanisi katika kuuza biashara au huduma yako. Idadi kubwa ya watumiaji wa YouTube inaweza kukupa wateja wa kutosha kama utakuwa na maudhui yenye ushiriki.

  1. Tumia mitandao ya kijamii kama LinkedIn

LinkedIn ni jukwaa la kuunganisha taalama mbalimbali. Na ndio maana jukwaa hili pia linatoa nafasi nzuri ya kushiriki maudhui yanayohusiana na biashara. Jukwaa la LinkedIn linakuwezesha kuonyesha ujuzi wako ndani ya sekta yako. Uhusiano wako na wanachama wengine wa LinkedIn utakuapa nafasi ya kutengeneza ushirikiano katika machapisho yako na taarifa zako. bure. Karibu nusu ya trafiki zote za mitandao ya kijamii zinazoingia kwenye maeneo ya kampuni ya B2B inatoka kwenye mtandao wa LinkedIn.

  1. Andaa au zungumza katika Makongamano mablimbali

Sawa na mitandao, kuzungumza kwenye matukio kuhusu mada kuhusiana na sekta yako ni njia nyingine ya kuonyesha ujuzi wako. Kutoa hotuba yenye kuchochea mawazo na yenye nguvu watavutiwa na wewe na biashara yako. Ambapo inaweza kuongeza ufahamu wa bidhaa na kuthibitisha biashara yako inafaa ili kukabiliana na changamoto za walaji.

Kwa kuanza, anza kutafakari mada tofauti na kujitolea katika matukio mbalimbali yenye kutengeneza mtandao mkubwa pamoja na makongamano makubwa ya biashara. Hii itakutengenezea uaminifu kwa walaji wa  biashara yako.

  1. Weka Vipeperushi katika sehemu Mbalimbali

Kuweka vipeperushi katika maktaba ya ndani, maduka ya kahawa, na biashara mbalimbali. Hii ni njia pekee ya masoko, ambapo watu hutumia muda mzuri katika hilo. Unaweza kutengeneza vipeperushi (Brochures and Flyers) vya bure kwenye PowerPoint. Kulingana na sekta yako, inaweza hata kukusaidia kufikia mteja bora: kama wewe ni mtaalamu wa viungo, kwa mfano, huenda unaweza kutoa vipeperushi kwenye vituo vya ndani au hospitali za karibu.

Hivyo basi unaweza kuanza kutimia njia hizi na baadhi ya nyingine nyingi kama sehemu yako ya kutafuta masoko ikiwa tu una bajeti ambayo haikidhi. Kwa msaada zaidi Bonyeza HAPA kupata ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kutumia njia hizi na nyinginezo.